Taratibu za kupata chanjo ya Hepatitis B kwa mkoa wa Dar es Salaam

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Jana niliweka topic hapa inayohusu chanjo ya Hepatitis B. Maswali yamekuwa mengi PM na mimi muda wa kumjibu kila mtu sina wakuu.

Basi naomba niweke majibu hapa japo wenzangu watajazia. Hepatitis B ni ugonjwa wa virusi kama UKIMWI na unaambukizwa the same kama ngoma. Hauna tiba sema bahati nzuri una kinga, kinga ambayo ndo tunayohamasishana humu kwenda kupata.

Kwa ufupi

Kama upo Dar kwa urahisi zaidi nenda Ocean Road hospital. Utalipia elfu kumi kwa ajili ya kupata vipimo. Kumbuka hupewi chanjo kabla ya kupimwa kama una maambukizi ama lah!

Ukukutwa na maambukizi utapewa ARV, kama huna utalipia tena elfu kumi na utachomwa sindano ya kwanza ya chanjo na utapangiwa tarehe nyingine maana sindano ni tatu.

Hiyo process ni kama masaa mawili tu.

Kwa mikoa mingine naomba wadau wengine waseme then tutaupdate
 
Vipi naweza tumia bima ya afya?
 
huu mradi hauna tofauti na mkrabita au mkukuta.
 
asante kwa taarifa mdau. nitasogea hapo ocean road
 
Wale wa tegeta, kunduchi,kutakua na huduma hiyo tareh 7 mwezi huu KKKT Bethania..kuliko kuenda mpaka Posta.
 
Huu ni Mradi tu wa kutengeneza hela! Hamna lolote pale...

Wanajifanya kuipa promo Hepatitis B kila kona kumbe wana Masanduku yao ya chanjo na reagents za Vipimo wanataka kuuza.
 
JF bana,wengine wana sema promo, wengine wanaogopa kupima kwakuwa wanahofu kuwa ngoma nayo inapimwa,lakini all in all mleta mada ana nia njema,ujumbe umefika usijesema tu hukuwa na taarifa siku ukipata maambukizi...
 
Hizo ARV wanazotoa, sasa mtu atajuaje exactly ana maambukizi ya huo ugonjwa wa ini?
Maana isije kuwa mtu wanampata na HIV then hawamwambii, wanamwambia ana hiyo Hepatitis B!
Now ukiwa unatumia ARV perception iliyopo ni moja kwa moja una ngoma!
Labda tueleweshane hizo ARV ni tofauti au lah, maana kunaweza kuwa na wimbi kubwa la unyanyapaa!
...halafu hii kitu mbona awali haikuwepo, kivile...takwimu za huu ugonjwa zipo vipi?
Kama huu ugonjwa ni hatari sana kiasi hicho, basi serikali iingilie kati itoe chanjo free, mbona ilichanja chanjo za mabusha free?!! na nyinginezo...
 
Arv ndo hizo hizo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…