Taratibu za kuvunja ndoa bomani

Taratibu za kuvunja ndoa bomani

jonas255

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
225
Reaction score
110
Habari wana JF

Mimi nilifunga ndoa ya bomani, ila ndoa yangu iliingia doa na uwezekano wa kurudiana imeshindikana.

Nilikua naitaji kujua taratibu za kuvunja ndoa za bomani, maana sheria inataka ndoa za Kiislam tu ndio zivunjwe mahakamani, ila za Kikristo na za bomani hazijazungumziwa.

Asanteni.
 
Habari wana JF

Mimi nilifunga ndoa ya bomani, ila ndoa yangu iliingia doa na uwezekano wa kurudiana imeshindikana.

Nilikua naitaji kujua taratibu za kuvunja ndoa za bomani, maana sheria inataka ndoa za Kiislam tu ndio zivunjwe mahakamani, ila za Kikristo na za bomani hazijazungumziwa.

Asanteni.

Kwa kawaida na kisheria Ndoa zote zinavunjwa na Mahakama kwa nchini Tanzania. Ukisoma kifungu cha 99, Cha sheria ya Ndoa Juzuu Namba 29 /2002, Kila mwana ndoa anahaki ya kuomba kuvunja ndoa yake Mahakamani kwa kupeleka maombi Mahakamani. Na hapa haijalishi ni ndoa iliyofungwa vipi,, ? hata ikiwa ya Bomani. Na Mahakama itavunja ndoa tu ikiwa itathibitika kwamba ndoa hiyo kweli haiwezi kurekebishwa,(the marriage has been broken irreparably).
TARATIBU ZA KUFUATWA

  1. Kwanza ni lazima mwanandoa anayetaka kuvunja ndoa awe na sababu za Msingi zinazonyesha kwamba ndoa kweli imevunjika na haiwezi kurekebishika. Mfano wa sababu za kuvunja ndoa zinaweza kuwa,,, Umalaya wa mwanandoa mwenza, ukatili hapa kipigo inaweza pia kuwa alama ya ukatili huo, kutelekezwa kwa mwanandoa.
  2. Lazima mwanandoa aanzie Baraza la usuluhishi la ndoa, kwa kupeleka malalamiko yake huko, inaweza kuwa kanisani kwako,,Baraza la kata , au Baraza la usuluhishi la ndoa lililopo pale Wizara ya Ustawi wa Jamii.
  3. Lazima Miaka miwili iwe imepita tangu kufungwa kwa ndoa kati ya wana ndoa.
  4. Akishapata karatasi ya Baraza la usuluhishi ambayo inasema wameshindwa kusuluhisha hiyo ndoa, ndipo anaweza sasa kufungua kesi Mahakamani kuomba kuvunjwa kwa ndoa. Na hapa inaweza kuwa Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu mkaazi, au Mahakama Kuu ya Tanzania.
  5. .Mambo ya muhimu wakati wa kuvunja ndoa ambayo pia Mahakama itayaangalia ,, ni matunzo na nani ataishi na watoto, Mgawanyo wa mali kwa wanandoa.

Haya ni kwa kifupi ,,kama bado hujatosheka mtafute mwanasheria aweze kukuongoza katika haya,,kwa sababu kuna kitu kinaitwa in every general Rule there is Exception.
 
Back
Top Bottom