Taratibu za Tender

Taratibu za Tender

Kiukweli hakuna jinsi tumia hela upate hela
Mimi mwenyewe hizi kazi za tenda ndizo zinaniweka mjini kwa kiasi fulani lakini sioni shida kumwelekeza mtu kisha vingine afanye mwenyewe.
Power of Attoney we hawa jamaa watafutie tu hela yao lakini bado pia wanatoa huduma hii kwa nafuu na wakati mwingine wanaweza kuamua kukusaidia bure kabisa si wakazaji kivile japo wakisimamia shoo wanaweza kukupiga kwa asilimia ya tenda lakini wengi hawako hivyo.
kuna kazi zingine zinahitaji bank gurantee nyingine unafanya ila uzoefu unaonyesha benki ni kazi kukukopesha moja kwa moja kwaajiri ya tenda vinginevyo unamtaji tayari na upo katika soko la bidhaa husika kwa muda mrefu lakini mwisho wa yote ni kwa jinsi gani unaweza kujenga ushawishi kwa benki husika ikiwa ni pamoja una uhakika wa biashara na kulipwa mapema.
Mkuu maandishi haya ni somo kubwa san kwetu kwa sisi tunaojitafuta kwenye hizi small startups zetu , Be blessed .
 
Mkuu maandishi haya ni somo kubwa san kwetu kwa sisi tunaojitafuta kwenye hizi small startups zetu , Be blessed .
asante Karibu.
Sio kila kitu unaweza kufanya lakini inawezekana unayo jinsi gani kinaweza kufanyika hivyo nafikiri ni vizuri ukawapa wengine ili nao wafanye ili hata ikitokea ukifa wakikatika kwenye kaburi lako wasione ni kaburi lililohifadhi mifupa mitupu bali waweze kujenga tafakari ya nini ulifanya kwao.
kwa pamoja tunaweza kufanikiwa.
 
Asante mkuu,

Naomba Pia unieleweshe kuhusu,
1. Kuhusu tender za manunuzi,
Ndio naanza, Sina mtaji pesa, Je bank wanaweza simamia show kwa mshindi Wa tenda then malipo yapitie kwao ili wajimegee na kinachobaki nikaishinacho?

2. Notorized attorney power, hiki kipengele nacho sijakielewa vizuri.

Mengi Sana mkuu natamani kuyafahamu Ila Kila ninapogusa kuulizia naambiwa nilipie maelekezo, Sasa Sina pesa
Power of attorney mbona ni rahisi sana mkuu, elfu kumi tu iandae then mpe mwanasheria akupigiee muhuri . Ukiwa na changamoto yoyote ya kujaza au kuandaa hizo tender docs nicheki nisimamie show, hata ukitaka nikafanye Lobb ili upate baadhi ya tender kwenye baadhi ya taasisi ndio mishe zangu hizo boss.

Malipo baada ya kazi
 
Umetisha Sana Mkuu,
Wewe tutaenda sawa, nitakucheki tufanye kazi
 
UPDATE :
Baada ya kupigiwa simu kuwa nimepata tender, nikaambiwa niwatumie Performance Securing Declaration, nikaingia website ya PPRA Nika saka sample ya hiyo doc, nikaipata, nikaedit, nikawatumia.
Wakaniambia leo atanitumia mkataba, nipo nasubir mkataba Sasa.

(Kwenye Mfumo wa Nest tayari wameniwekea Intention letter pamoja na Award letter)

Ahsante Sana kwa wote Munaoendelea kunipa Muongozo hadi pale nitakapo kabidhi hii kazi.
🙏🙏
 
Asante mkuu,

Naomba Pia unieleweshe kuhusu,
1. Kuhusu tender za manunuzi,
Ndio naanza, Sina mtaji pesa, Je bank wanaweza simamia show kwa mshindi Wa tenda then malipo yapitie kwao ili wajimegee na kinachobaki nikaishinacho?

2. Notorized attorney power, hiki kipengele nacho sijakielewa vizuri.

Mengi Sana mkuu natamani kuyafahamu Ila Kila ninapogusa kuulizia naambiwa nilipie maelekezo, Sasa Sina pesa
Kama utapass na kuwin Tender inabidi Usign mkataba wa kazi husika na ukishakuwa na mkataba unaweza kwenda Bank na kuutumia kupata Mkopo japo Bank zinatkfautiana utaratibu ila unaweza kuanza na ivo alafu utajua utaratibu wa Bank husika.

Notorized power of Attorney hii nguvu au wajibu anaopewa Mhusika wa kampuni katika mkataba husika kama kusign Documents zote za mkataba, kufanya negotion za bei za huo.mkataba, kuhudhuria vikao kuhusu huo mkataba kwa kiufupi huyo anayepewa iyo POA ndio anakuwa signatory wa huo mkataba na sio mwingine
 
UPDATE:
Leo nimepigiwa simu muda wa saa nne asubuhi na nimeambiwa nimeshinda tender ambayo niliomba, ila Sasa toka mda huo sijaona update yeyote kwenye Mfumo (NEST)
Je, niendelee kutulia nikisubiri update za kwenye Mfumo au hatua hii na kuendelea Mfumo hauhusiki?
Wasiliana na PMU mara nyingine mfumo unachelewesha mambo
 
Tuna group letu la kupeana uzoefu mambo ya tender wadau , mimi ni mmoja wapo wa niliefanya hizi issue sana tu . kuna wazoefu pia zaidi tunapeana moja mbili tatu, kama utapenda kushiriki nasi utupe mawazo ni PM nikupe link
 
Power of attorney mbona ni rahisi sana mkuu, elfu kumi tu iandae then mpe mwanasheria akupigiee muhuri . Ukiwa na changamoto yoyote ya kujaza au kuandaa hizo tender docs nicheki nisimamie show, hata ukitaka nikafanye Lobb ili upate baadhi ya tender kwenye baadhi ya taasisi ndio mishe zangu hizo boss.

Malipo baada ya kazi
Nitakutafuta mkuu tuyajenge.
 
Kirefu cha PMU ni nn? Ofisi zao zipo wapi?
ukenda kwenye hiyo taasisi uliyoomba hiyo tender uliza Procument Unit au ofisi za manunuzi watakuonyesha. Ukifika elezea tru watakwambia anni anahusika na hiyo Order
 
Back
Top Bottom