Taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu mwalimu kufanya biashara darasani kwa wanafunzi anaowafundisha?

MoR 91

Member
Joined
Mar 19, 2017
Posts
84
Reaction score
132
Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
 
Hakuna cha kujadili hapo Mkuu. Wape watoto hela au waambie hela za kuwapa huna ila make room ya kuwapa breakfast kabla hawajaenda shule. Watoto ni waelewa na wasikivu, unavyomlea ndo anavyokuwa akiyashika hayo. Walimu wanafanya hivyo kuokoa maisha yao.
 
CCM haijawapandisha walimu madaraja wala haitaki kuwapa posho unategemea nini? Waache walimu wapambanie familia zao,kwani wana hali ngumu sana.Wape watoto 200 waende nayo shule,hakuna shule bila visheti, maandazi, vibama etc
 
Wape watoto hela wakanunue maandazi ili wasome wakiwa wameshiba,
Sidhani kama Mwalimu kuuza maandazi ina athari kwenye kutimiza majukumu yake,

Nilifikiri ungelalamika kua kiwango cha uelewa au ufaulu kimeshuka kwa wanao,kumbe unalalamikia kwa kuombwa hela ya maandazi na mtoto wa chekechea!

Mwalimu kajiongeza ili kupunguza ukali wa maisha,pia nina uhakika uongozi wa Shule wanaijua hiyo biashara yake,kungekua na madhara katika kutimiza majukumu yake wasingemruhusu.
 
Achana na kuwaza vya sera sijui nini wape watoto hela za maandazi mkuu. Usitafute sympathy kwetu.

Sasa wewe pima tu, kama huna mia mia za kuwapa asubuhi warudishe mpanda wakasome huko wakae na bibi yao we kaa morogoro
 
Ngoja aje Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI Mpwayungu Village atoe ufafanuz(hapa natania tu). Kiukweli kuna nyuzi nyingi humu watu walitoa kuashauri walimu wajaribu kujiwekezea katika biashara zingiine na ndio maana leo kuna walimu wanamiliki bodaboda,siku za wekeend anapiga kazi ya bodaboda,ila la kuuza maandazi darasani hii inaonesha ni jinsi gani walivyochoka
 
Achana na kuwaza vya sera sijui nini wape watoto hela za maandazi mkuu. Usitafute sympathy kwetu.

Sasa wewe pima tu, kama huna mia mia za kuwapa asubuhi warudishe mpanda wakasome huko wakae na bibi yao we kaa morogoro
Sikupingi unachokifikiri , maana najua uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo

Huna Cha kushauri Kaa kimya si lazima uchangie
 
Wape watoto hela wakanunue maandazi ili wasome wakiwa wameshiba,
Sidhani kama Mwalimu kuuza maandazi ina athari kwenye kutimiza majukumu yake,

Nilifikiri ungelalamika kua kiwango cha uelewa au ufaulu kimeshuka kwa wanao,kumbe unalalamikia kwa kuombwa hela ya maandazi na mtoto wa chekechea!

Mwalimu kajiongeza ili kupunguza ukali wa maisha,pia nina uhakika uongozi wa Shule wanaijua hiyo biashara yake,kungekua na madhara katika kutimiza majukumu yake wasingemruhusu.
Uko sahihi mkuu lakini nafikiri kwanza ungetofautisha kulalamika na kuuliza ,
Hakuna mahli nimelalamika hapo Bali niliuliza kutaka kujua tu kama ni sahihi au si sahihi
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Acha ubahili wewe, wape wanao hiyo 200 wakale maandazi
 
Back
Top Bottom