Taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu mwalimu kufanya biashara darasani kwa wanafunzi anaowafundisha?

Watoto wadogo hawanaga uvumilivu kabisa linapokuja swala la njaa, kibaya zaidi akiwa na Hela mfukoni akili yake yote inahamia Nje ya darasa.
Lakini Mkuu hata nyie kwenye maofisi yenu huko Kuna tozo zisizo rasmi nyingi tu.. Wape watoto Hela hayo mandazi hayawezi kumtajirisha Mwalimu kiasi Cha Kuja kumfungulia Uzi hapa
 

Acha ubahili wewe, wape wanao hiyo 200 wakale maandazi
Sawa mkuu ila hujanielewesha miongozo na kama hujui kama Mimi Kaa Kwa kutulia tusubiri wenye kujua watufahamishe
 
Kuna ubaya kutaka kufahamishwa sera za Elimu ikiwa Mimi ni mdau pia wa sekta hiyo ?
 
Haya ni matunda ya kuongozwa na CCM na hii tabia haijanza leo. Ni ya siku nyingi kabisa. Na kama hujui, wameenda mbali zaidi na kufanya hao hao wanafunzi ndiyo wauzaji wao. Yaani kama ni maandazi, basi mwalimu anamkabidhi mwanafunzi mmoja awe ndiyo muuzaji wake.
 
Uko sahihi mkuu lakini nafikiri kwanza ungetofautisha kulalamika na kuuliza ,
Hakuna mahli nimelalamika hapo Bali niliuliza kutaka kujua tu kama ni sahihi au si sahihi
Ndani ya uzi wako yapo malalamiko pia,
Umelalamika kua, Kuna mabadiliko ya kitabia kwa wanao kuomba pesa asubuhi wanapotaka kwenda Shule.
 
Kamba ya Mwalimu inafika darasani au haifiki? Hilo ndiyo la kujiuliza.
Kingine darasa bila ya biashara za waalimu hata halinogi watoto wanaweza wakadhani wapo international school
 
Nina uhakika kabisa ninakuzidi uwezo wa kufikiri kaa ujue hivyo tu
Unaonyesha ni jinsi Gani ulivyomkulupukaji , wapi nimeandika kuwa ninakuzidi katika uwezo wa kufikiri?
Au nimeandika kuwa una uwezo mdogo wa kufikiri ? Usiongozwe na mihemko mkuu soma elewa kilichoandikwa kabla hujajibu
 
Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?
Anza kwanza kuuliza kwa nn Mawaziri, wabunge, makatibu wakuu na viongozi wengine waandamizi wanafanya biashara na serikali ikiwa taratibu haziruhu, ukipata jibu uendelee na hilo la walimu!!
 
Mimi nafikiri mwalimu amejiongeza na kuamua kuwafundisha watoto ujasiriamali kitu ambacho watoto wetu hawafundishwi lakini cha muhimu sana hasa wakati huu ambapo ukosefu wa AJIRA RASMI ni mkubwa mno. Heko mwalimu badala ya kuwafundisha watoto kuhesabu miguu ya jongoo, kuchora panzi ,kuchinja vyura nk umeamua kuwafundisha ujasiriamali kwa vitendo. Pia ndugu yangu acha ubahili wape watoto pesa kidogo, tena waweza kuwapa ya wiki nzima uone jinsi wanavyoweza kutunza fedha.
 
πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±
 
Blaza unataka walimu wakale kwenye siasa? Au kanisani? Imeandikwa Kila mtu ale madhabauni kwake
....kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake...
Ila tukubali kwamba tukiendelea na tabia hizi za kuruhusu mambo ya uvunjaji wa kanuni,miongozo,taratibu,maadili na sheria za kazi,tutaendelea kuwa na taifa lenye wafanyakazi wasio na weledi mahala pa kazi kama ambavyo tumekuwa tukilalamika mara kwa mara juu ya wafanyakazi na wayatendayo mahala pa kazi.

Samaki mkunje angali mbichi.

Tukubali moja,ama turuhusu hizi tabia na tusilalamike, au tukataze na kutengeneza uwajibikaji mahala pa kazi na weledi na kufaidi matunda yake.

Tanzania bora ya kesho inaanza kujengwa leo na watoto wanaokuzwa kimaadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…