Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. DUNSTAN KITANDULA - TARATIBU ZIFUATWE TWIGA CEMENT KUINUNUA TANGA CEMENT
Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Tanga, Mhe. Dunstan Luka Kitandula wakati anachangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara amesema kuwa watu wa Tanga hawatakuwa tayari kuona Tanga Cement inageuka kuwa Godwon na kuwa hawapingi Twiga Cement kuinunua Tanga Cement ila utaratibu ufuatwe
"Kama kuna maamuzi yaliyoamriwa kisheria tusikiuke maamuzi hayo, tukiendelea kukiuka maamuzi ya vyombo vyetu vya kisheria tunapeleka ujumbe kwamba tusitumie mahakama zetu za ndani, mashauri yote yakaamriwe nje. Hii si sawa" - Mhe. Dunstan Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga
"Hivyo hatutakuwa tayari kuona Tanga Cement inabinafsishwa na kugeuka kuwa godown na kisha kuja kuchukua malighafi Tanga na kwenda kuzalisha Dar es Salaam. Hilo hatulitaki na hiyo ndio hofu yetu watu wa Tanga" - Mhe. Dunstan Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga
"Hatupingi Twiga Cement kuinunua Tanga Cement, tunachosema taratibu zifuatwe, watu wa Tanga ni wahanga, tumeshang'atwa na nyoka, tukiguswa na majani tunastuka. Tanga tulikuwa na viwanda 8, baada ya kuvibinafsisha vimegeuka kuwa magofu, havifanyi kazi" - Mhe. Dunstan Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga