Taratibu zipoje kulipa deni la Marehemu?

Taratibu zipoje kulipa deni la Marehemu?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
Ndugu zangu habari za jioni?

Naomba ushauri wa kisheria mdogo wangu anayenifata amefariki alikiwa ni mtumishi wa serikali wilaya x, jana mida ya jion siku 4, baada ya mazishi nimepigiwa simu. Na wafanyakazi wa MABOTO COMPANY, kuwa marehemu alikopa fedha, sasa wanataka msimamizi wa mirathi awasaidoe kurejesha yaani kulipa deni.

Nilibishana nao sana, nikiwa na ufahamu mdogo kuwa mkopo unapotolewa huwa unakuwa na bima ya majanga, endapo muhusika akifariki, akiacha kazi basi bima hiweza kufidia. Na kuwaambia kuwa mirathi ni kwa ajili ya watoto wa marehemu na wazazi wa marehemu na sio kulipa madeni.

Madeni yote kwa mujibu wa sheria ya mkopo ya B. O. T, yatalipwa na kufidiwa na bima ya mkopo, na mdhamini ni mkurugenzi mtendaji na sio vinginevyo. wakaanza ooh unajua kiubinadamu tunatakiwa tukae tuliangalie kwa chochote kile mfidie.

Je kwa hili limekaaje?
Naomba Muongozo.
Maana naona hapa kuna uhuni unataka kufanyika
 
Sio mikopo yote , mzee wangu alipofariki alikuwa na deni Acces bank. Familia tulilipa. Kikubwa omba mkataba wa mkopo walioingia nao marehemu usome ndio utapata majibu familia mnapaswa kulipa au kutolipa.
 
Nimewaomba, mkataba wanazungusha zungusha hawaeleweki, mara wanasema tuje tuongee kirafiki mi nimewaambia mdhamini wake alikuwa mkurugenzi hivyo waanzie kwa mkurugenzi
 
Huyo si alikuwa mtumishi na mdhamini wake si anajulikana? Hao ni wahunì ati muongee kirafiki? Ndugu yenu kashakufa watajua wenyewe. Staki kuiongelea kisheria coz najua kuna uhuni unaendelea hapo na mkataba hawawezi kuwa nao. Wanyamazie tuone mwisho wake.

N.b ikitokea wakamstaki msimamizi wa mirathi ni sawa utaratibu ufuatwe. Tho yawezekana marehemu hajaacha vitu ambavyo vinaweza lipa mkopo huo, ndo itakuwa imeisha hiyo.

Kuna watu baada ya mtu fulani kufa wakatengeneza ma docs ya kutosha ya mkopo + kiwanja miaka 3 nyuma na kufoji sain ya marehemu. Na wadhamini walikuwa washikaji zake, mke etc. mahakamani waliona aibu ile saini ya marehemu ilitengenezwa aiseee almost ikawa kama ya marehemu.

Signature ya mke wake waliweza kuipatia maana ilikuwa simple picha zote zilikuwepo in short kwa kuangalia zile docs zinaendana na ukweli.
Mke wake alijisimamia akasema mme wake hakuwahi kuwa na shida ya kuchukua mkopo.
Ushahidi ukaletwa Signature za marehemu kama zinafanana, mke wake akasema hapana akaleta kitambulisho cha nida mweee you people shoud have unique signatures.

Signature ya marehemu kuna jinsi mwisho alikuwa akiikunja afu kuna kama ka star hiyo walishindwa ikopi.

Case inaendelea ila hawafiki popote wale nyau.
 
Sio mikopo yote , mzee wangu alipofariki alikuwa na deni Acces bank. Familia tulilipa. Kikubwa omba mkataba wa mkopo walioingia nao marehemu usome ndio utapata majibu familia mnapaswa kulipa au kutolipa.
Wakitengeneza mkataba Mpya yaani wakiforge inakuaje?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Nimejifunza jambo moja. Nisidedi nikiwa na deni.....
 
Hamna maongezi hapo, inaonekana on their part hawakufuata taratibu , kazia hapo waende kwa mdhamini
Nimewaambia ili niwapokee waje na barua ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya inayoelezea kuhusu deni la marehemu vinginevyo siwalipi hela itaenda kwa watoto wa marehemu tu na sio vinginevyo MABOTO MICROFINANCE wanataka kuleta janja za ajabu
 
Wakitengeneza mkataba Mpya yaani wakiforge inakuaje?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Mkataba wa mikopo lazima uwe na mdhamini ni ngumu kuforge na mdhamini lazima atambue mashart ya mkopo husika , sisi ilikuwa rahisi mdhamini alikuwa bi mkubwa kwahyo kila kitu alikuwa anaelewa . Kikubwa tuliwaomba hatutalipa kwa mtiririko kama aliokuwa analipa marehemu tutazilipa kwa pamoja baada ya kupata haki za marehemu za kiinua mgongo walielewa.
 
Sio mikopo yote , mzee wangu alipofariki alikuwa na deni Acces bank. Familia tulilipa. Kikubwa omba mkataba wa mkopo walioingia nao marehemu usome ndio utapata majibu familia mnapaswa kulipa au kutolipa.
Inawezekana na nyie mlilipa kwa mihemko! Mlikuwa mmejiridhisha kwamba mkopo haukuwa na Bima?
 
Inawezekana na nyie mlilipa kwa mihemko! Mlikuwa mmejiridhisha kwamba mkopo haukuwa na Bima?
Ndio tulijiridhisha na mdhamini alielezwa pia mdhamini alikuwa ni mama, taratibu zao ukifa deni litafidiwa na mali za marehemu, alizoziweka dhamana kama mdhamini au familia wakishindwa kulipa kwahyo ilibidi familia tupambane na haikubaki pesa nying sana yeye mwenyewe alishausogeza .
 
Poleni kwa kweli! Hiyi benki ni ya kuepuka, maana mara nyingi huwa tunalipa Bima ya mkopo na imeelezwa kabisa ni kwa ajili ya nini?
 
Asante, tuliopo hai tujifunze tusiwape tabu familia zetu tunapoondoka. Tuangalie na taasisi za kukopa
Muhimu sana unapokopa kujua kama mkopo unaochukua unabima au la vinginevyo unaweza kuacha deni kubwa kwa familia lisilobebeka
 
Urithi ni pamoja na madeni, kama marehemu alikuwa anadaiwa, msimamizi wa mirathi ndo atalipa hayo madeni, ila unalipa kutoka kwenye mali za marehemu, sio mali zako binafsi, tena madeni ndo yanatakiwa yalipwe kwanza alafu kinachobaki ndo utagawia warithi, sheria iko hivyo.
 
Back
Top Bottom