Nifahamisheni kuhusu hizi signal zinavyotolewa.. Kwa mfano huyo bwana Oleg anaenda supermarket na mfuko wenye ujumbe kwa M16 na hao M16 wanamfuko wenye maandishi yakupokea ujumbe.. Swali! Wamejuaje kama Leo kachero Oleg atatoa ujumbe? Na Oleg atajuaje Kama Hawa jamaa watakuwepo hapo? Au ni maeneo aliambiwa watakuwepo hapo anytime na mifuko yao wakumsubiri Oleg?
Kwa ufaham wangu huyu Oleg, hakuwa agent Mi6 wakt anapelekwa katika ubalozi wa Russia nchini Denmark. Maana Oleg, baba yake pia naye alikuwa KGB officer. Oleg akiwa Denmark, alichukizwa na matendo ya Russia dhidi ya Czech, ndipo yalipelekea kubadili nia yake ya kuwa mtiifu kwa Russia. Simu yake moja aliyoipiga kwa mkewe kuonyesha kuchukizwa na kitendo hicho cha Russia dhidi ya Czech ndio ilitoa signal kwa shirika la intelligence la Denmark kwamba huenda Oleg anataka kuwa double agent.
Denmark kwakua hawakuwa na skills za kumtongoza a high ranking official na intel officer katika embassy ya russia, wakawaomba wabia wao Mi6 wawasaidie Kwenye hilo. Kwahio hapa, ndipo Mi6 ilimnasa baada ya vikao kama viwili, cha mwisho alicho insists (Oleg) kuwa, yupo tayr kwa kuongea nao nq kuwa double agent kwa sharti moja tu kikao kinacho fuata atakutana na maafisa waingereza pekee bila kuwepo raia yyte wa Danish.
Alifanya kazi na Mi6 nadhani kwa miaka 4 hivi kwa ku leak top Russian secrets kama micro films za raia wa Russia walio majajsusi Europe, pia maafisa na raia wa Europe wanaoifanyia kazi kwa russia. Baada ya miaka minne, alirudishwa russia makao makuu kgb. Akiwa russia alikuwa deskman ndiye ana handle docs zote za siri za Europe yote nk.
Baada ya miaka minne kuisha akiwa Russia, alipewa post ingine, safari hii alipelekwa London kwy ubalozi wa russia. Hapa ndio alifanya maangamizi makubwa zaidi kwa russia. According to Charles Powell, ambaye alikuwa mshauri wa usalama na katibu wa waziri mkuu wa wakati huo Magret, anasema "there was nothing more secret in uk than the existence of Oleg and who he was". Mawaziri wala nani, hamna aliemjua labda maafisa wa juu wa Mi6.
Awali akitokea Denamk na kurudishwa russia, kwa upande wao mi6 hawakufanya any attempt ya kuwasiliana naye, ila walimpaga Oleg namb maalum ya simu ya ku initiate mazungumzo wakati wowote wanapo potezana. Pia walipeana signal ya kushika plastic bag, sehm moja maalum nchini russia wakt wowote ikitokea anahisi anafuatiliwa na anahitaji atoroke. Na ili kujibu hii signal, ofisa wa Mi6 atattokea kutoka kwny crowd huku ana kula brand fulani ya chocolate, kama majibu kuwa ameeleweka.
Katika mission zake zote hizo abroad hakuwa na mkewe, na hata siku anatoroka pia alimficha mkewe kuwa anatoroka.
Kufuatia Speeches za Reagan kuhusu nuclear, na ile pressure iliokuwa kubwa kuwa mda wowote vita ya nuclear itaanza, ilfanya russia ihisi kuna mtu ndani yao anatoa siri. Kumbuka kuwa CiA walikuwa wakipewa intel kwa kile walichokiita " drip fed information on need to know basis" kutoka kwa wabia wao Mi6, swala ambalo hawakulifurahia. Walitaka direct intel from the source.
Kufuatia hali hiyo CiA wakampa kazi mkuu wao wa CiA counter russia, ya kufuatilia source ya high class info wanazopata mi6 na kuwapa wao. Ila ambacho CiA hawakakujua ni kuwa huyo afisa wao, Naye ni agent wa KGB. Huyu afsa ambaye baade CiA walimshtukia, alipopewa kazi hiyo na ili kutoonekana alikuwa compromised, alivujisha document Kibao ikiwepo hisia zake kuwa a newly appointed boss katika embassy ya Russia jijini London ambaye ni Oleg ndio source ya uvujishaji.
KGB walipoliona Jina lake katika ya majina mengi kutoka kwa source yao ndani ya CIA, wakamwita Oleg arudi nyumbani haraka on pretext ya kupewa promotion. Oleg chale zilimcheza, ila alijua kukaidi direct order kurudi russia itaonyesha wazi kuwa yupo guilty na angeshughulikiwa.
Alirudi russia bila kuwaaga mi6. Alipofika haraka sana walimpeleka kwny jumba lao, wakamtilia sumu ya kumlewesha, wakamtocha lakn uzuri wake Oleg hakutoa siri ya uhusika wake na Mi6. Basi kgb wakaamua kuchenj tactics kwa kumpa house arrest, na hapa ndipo baadae alitoroshwa, nadhani kwa operation ilioitwa piplico ..