Tanki
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 538
- 246
Jumamosi tarehe 24 natakiwa nisafiri niende MOROGORO / TURIANI kumalizia msiba wa mzazi wangu. Then bado kuna vitu havijakaa sawa. Then sina kazi kwa sasa. Sasa, baada ya kufuatilia mafao yangu ya NSSF (Fao la kutokuwa na ajira kwasasa) tarehe ambayo NSSF walinipangia kwamba nitakuwa nimepata pesa zangu ni tarehe 23, yaani siku tatu tu zimebaki. Na tegemeo langu lote lipo kwenye hiyo hela ya NSSF.
Kwenye app ya NSSF tangu wiki iliyopita nikiangalia Salio kwasasa unasoma ZERO, wakati hapo awali pesa ilikuwa inasoma. Na nikiangalia michango yangu nayo tangu wiki iliyopita itaonyesha ZERO ZERO, (No data available) ila pesa nikiangalia kwenye bank NMB hakuna pesa.
Wakuu, hapa naiwaza hiyo tarehe 23 siku tatu kutoka leo, je hiyo hela itaingia? Maana nimeshafuatiria sana. Mara jina lilikuwa na herufi tofauti, mara tarehe ya kuzaliwa zilipishana, nilifuatilia na kukamilisha vyote hivyo.
Maombi yenu waku, maana hiyo tarehe wasiponiwekea hiyo hela aisee aisee aisee sipati picha.