Tarehe 24 Novemba, 2019 kiza ni kinene na dunia masikio yapo Tanzania

Tarehe 24 Novemba, 2019 kiza ni kinene na dunia masikio yapo Tanzania

TumainiEl

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
7,280
Reaction score
14,342
Sijui ni za kunyapia nyapia ama kweli ila uchaguzi Serikali za mitaa ni zaidi ya Korosho wenye akili zinawauma japo yaliotokea Zanzibar yanaweza kufanyika hapa kwetu.

Japo yakifanyika mjue mabeberu watajibu kwa silence ya ule usiku wa Yesu kufufuka. Fukuto hili litaendelea mpaka uchaguzi 2020 jambo nihatari sana kwa ustawi wa taifa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Why Wazungu wana akili sana watakchokifanya baada wakujua uchaguzi huu tumejipa goli basi watapunguza misaada ya maendeleo kwa phase by phase jambo litaleta msoto na kutafutana pamoja na kupunguzana na ndio maana nawausia Watanzania kama tuna macho ya rohoni tusali miaka mitano ijayo ni mikali sana kuliko sasa.

Uchaguzi nizaidi ya kiza kinene

Update
Kil kilipangwa. Kimefanikiw. Kiukweli tusali Mungu aiku Tz
 
Mnapoteza muda wenu. Iq ya magufuli ni sawa na wa zungu 1000 relax hakuna kitakachotokea
 
Kikubwa cha kujiuliza, kwa nini iwe hivyo? Tuna sababu ya kulazimika kupita kwenye njia hii? Ni nini hasa? Ni kukosa utashi? Ni uroho wa madaraka? Ni kukosa maono? Ni ushamba? Au basi tu mtu kazaliwa na roho ya shetani?

Dunia hii ambayo siku za kila mtu zinahesabika. Dunia ambayo kila aliyeumbwa amepata hiki na kukosa kile. Dunia ambayo sote tuliomo hakuna mwenye roho ya chuma. Kwa nini usitende kwa unyenyekevu, ukatimiza wajibu wako, na ikiwa wengi wakasema, hapana, ukajiondokea kwa amani, ukakaa pembeni, nawe ukahudumiwe na wengine?

Utatenda nini katika ulimwengu huu ambacho wengine hawajawahi kutenda? Iwe ni uzuri kuna waliotenda mazuri kuliko wewe lakini walipita. Iwe ni ubaya, wapo waliowahi kuwa wabaya kuliko wewe lakini wakapita. Kama ni ukatili, uharamia, ubabe, kujiamini, kutojali - ujue wapo waliokuzidi lakini mwisho wa yote waliiacha Dunia ikiendelea kuwa ya mviringo, wakaondoka kwenye hali ya unyonge wa pekee.

Ukipata nafasi tenda uwezayo, mwombe mola wako abariki uyatendayo ukiamini wewe si chochote si lolote katika mamilioni ya unaowaongoza.
 
Hahahah dah! Kwahio hawa jamaa wanakuja Bongo?? Vikwazo vinafannanaje?
Siku vikija ndiyo utavijua. Hata Burundi utaiona mbingu. Nimefika Zimbabwe, hakuna kinachoenda. Chochote unachokifikiria hakitakuwa na maana. Wala usiombee. Hata ambao hawajawahi kwenda mkoa mwingine, watatafuta nchi ya kwenda.
 
Kususia uchaguzi nako ni K NA CCM ilivyo uchaguzi utafanyika na hakuna kitakachotokea kwani ZENJI ilikuwaje? Mbona mpk Leo kimya?
Usilinganishe Zanzibar na Tanganyika. Huwezi kuiwekea vikwazo Zanzibar vikafanya kazi bila ya kuiwekea vikwazo Tanganyika. Hakuna mwenye akili anayeweza kufikiria kuiadhibu Zanzibar bila ya Tanganyika.

Kamba hukatikia pembamba.

Tukikosea kidogo tu, Tanganyika itabeba mpaka adhabu ya Zanzibar.
 
Kusali bila kuchukua hatua hakusaidii kitu, sala pamoja na kushughulika wenyewe kulibond kichwa joka.
unafiki na mapandikiz ndani ya vyma vya siasa ni kiza kinauyesa democrasia yetu na kwa hali ilivyo na utawala huu nibora kusali kuliko malumbano...
 
Hii mentality ya watu kukaa nyumbani wakitegemea mabeberu ndo wawafanyie mabadiliko ni ya kishamba mno.

Bolivia wamehitimisha utawala wa mtu kwa kumdindia wenyewe for weeks kama ilivyokuwa Sudan tu.
 
Usilinganishe Zanzibar na Tanganyika. Huwezi kuiwekea vikwazo Zanzibar vikafanya kazi bila ya kuiwekea vikwazo Tanganyika. Hakuna mwenye akili anayeweza kufikiria kuiadhibu Zanzibar bila ya Tanganyika.

Kamba hukatikia pembamba.

Tukikosea kidogo tu, Tanganyika itabeba mpaka adhabu ya Zanzibar.
Umenena vyema!
 
Siku vikija ndiyo utavijua. Hata Burundi utaiona mbingu. Nimefika Zimbabwe, hakuna kinachoenda. Chochote unachokifikiria hakitakuwa na maana. Wala usiombee. Hata ambao hawajawahi kwenda mkoa mwingine, watatafuta nchi ya kwenda.
Kwanini ccm wanang'ang'ania madaraka?
Why wasiwaache na wengine wakajaribu?
 
Back
Top Bottom