Tarehe mpya ya kuapishwa kwa Raila Odinga ni 30 Januari

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Baada ya kuahirishwa mara mbili, muungano wa Upinzani nchini Kenya umepanga kumuapisha kiongozi wao , Raila Odinga kama rais tarehe 30 Januari na Kalonzo Musyoka kama makamu wa rais.

Kituo cha Citizen Tv kinasema Odinga ataapishwa kwenye uwanja wa Uhuru Park kabla ya kufanyika kwa mikutano kadhaa

Kalonzo Musyoka ambaye ni mmoja wa viongozi wa upinzani alisema kama serikali haitafanya mazungumzo nao basi watajiapisha

Mwanasheria mkuu wa Kenya alionya kuwa kitendo cha kuapishwa Raila ni uhaini ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifo

Raila alisema yupo tayari kufa ili watu wapate kiongozi waliyemchagua

================================================

NASA’s much awaited swearing in of Raila Odinga and Kalonzo Musyoka has been scheduled for the end of this month according to a special planning committee. Citizen TV has learnt that the opposition coalition intends to swear in Odinga at Uhuru Park preceded by a series of rallies and meetings in several counties.


Source: Citizen Tv
 
Hawa jamaa wanaweweseka sana. Sasa mahakama iliwapa nafasi ya kushinda kupitia ballot box wao wakaingia mitini...sasa wanajiapisha kwa vigezo gani? Naona ukimchekea nyani utavuna mabua...ndicho kinachotokea. Uhuru hawa jamaa usicheke nao. Wape haki yao wanayoitafuta kwa nguvu.
 
hivi atakapo maliza kujiapisha ataelekea ikulu ya wapi? atatoa order kwa mkuu wa majeshi yupi? waafrika kwakeli sijui tu.
 
Raila ana hamu ya kufia jela kwa kosa la "uhaini". Anataka kujiapisha ili iweje sasa?
 
jamaa yangu Raila, njoo ni kushauri kitu.
 
Uraisi unaraha yake mtu hata akiwa milionea vp haridhiki na alichonacho hadi cheo hicho apate
Utajiri kumbe sio kitu kama cheo cha uraisi
 
hivi atakapo maliza kujiapisha ataelekea ikulu ya wapi? atatoa order kwa mkuu wa majeshi yupi? waafrika kwakeli sijui tu.
Mkuu uasi huanzia hapo, ukiona kiongozi anataka kujiapisha ujue ana jeshi lake liko msituni. Uhuru hapaswi kucheka kwenye hili.
 
Kinachowawasha Raila na malofa wenzake ni kwamba, kila anapoongea rais U.Kenyatta, wanangoja aongee kuhusu mipango yao lakini wapi. Hapo rais Uhuru nampa tick. Alishatoka kwenye 'campaign mode' sasa yupo kazini. Vichwa vitawauma sana.
 
Mkuu uasi huanzia hapo, ukiona kiongozi anataka kujiapisha ujue ana jeshi lake liko msituni. Uhuru hapaswi kucheka kwenye hili.
unekuwa raisi ungechukua hatua gani za haraka kudhibiti hali hii?
nadhani hapa ndipo uhuru anapopata kigugumizi ni hatua gani achukue lakini pia mpk mtu anatengeneza jeshi kimyakimya bila vyombo vyako kukupa nyeti basi nawewe uko hatarini.
 
Wanapoteza muda.Waunge mkono juhudi za Mh. Kenyatta za kuiendeleza Kenya na kujenga umoja wa kitaifa.
Hizi mbwembwe na porojo hazitawasaidia chochote.Sana sana, Kenyatta akichoka atam-sue kama mhaini tu.
 
Wanapoteza muda.Waunge mkono juhudi za Mh. Kenyatta za kuiendeleza Kenya na kujenga umoja wa kitaifa.
Hizi mbwembwe na porojo hazitawasaidia chochote.Sana sana, Kenyatta akichoka atam-sue kama mhaini tu.
Kenyatta ameiendeleza au kujenga Kenya wapi na wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…