Mbona ana mchecheto na kazi? Ngoja akajitie kimuhemuhe cha kufanya kazi kwa bidii atapunguzwa makali kibabe na wakongwe wa kazi atakaowakuta. Anauliza mshahara kwani wakati anaomba kazi hiyo hakujua ataanza kulipwa kiasi gani? Aache ulimbukeni atachekwa na kudharauliwa na wakongwe wa kazi