Tarimba ajiuzulu Yanga

Tarimba ajiuzulu Yanga

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba, ametangaza kuachana rasmi na wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Radio Uhuru, Tarimba amefunguka na kueleza kuwa kumekuwa hakuna maelewano baina yake na Makamu Mwenyikiti wa Yanga, Clement Sanga, ambaye ameivunja kimyakimya kamati hiyo ambayo ilipitishwa katika mkutano mkuu.

Kufuatia tukio la kuvunjwa kwa kamati, Tarimba amesema hawezi akawa na muda wa kuonana na Sanga kwasababu ameivunja kamati, na hata kama asingefanya hivyo asingekuwa tayari kutekeleza majukumu ya kamati hiyo.

"Waachane na mimi , mimi sina muda wa kuonana na Sanga waachane na mimi, yeye kwanza kamati kaisha ivunja na hata kama wasinge vunja mimi nisingeweza kufanya kazi nao" alisema Tarimba.

Mbali na kauli hiyo, Tarimba amekanusha uwepo wa taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kuwa kamati yake imelipa madeni ya fedha zote zilizokuwa ni malimbikizo ya madeni kwa wachezaji.

Tarimba ameeleza kuwa hakuna ukweli kuhusiana na hilo akiwahusisha viongozi wa Yanga kuwa wamekuwa waongo hivyo na kuwaomba waache masuala ya usanii kwa kuwa klabu hiyo ni taasisi kubwa.

"Wanayanga mnadanganywa Yaani wanayanga mnadanganywa mchana kweupe, Yanga tuna tamaduni zetu sio hizi, viongozi ni waongo ,nawaomba watulize akili zao wasaidie timu ,wengine ni wakubwa wanaongoza mpaka bodi ya ligi ,sasa watumie ukubwa huo kuipeleka Yanga mbele waache uongo uongo" alisema
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Bongo kuskumiana vitambi tu
Na kipgiana hon kwenye ranger Rover
 
Wanachama mmedharauliwa vya kutosha ..muondoeni Sanga haraka la sivyo yanajirudia ya msimu uliopita...hawataki kufanya mchakato wa ubinafsishwaji wanajua hawatabaki Yanga..aibu ya msimu uliopita inatosha
 
Sanga anacheza na akili za wanachama....kashajua wana mihemko na manji wakati manji hana mpango wa kurudi yanga...anachofanya anawadanganya kwamba manji anarudi ili kuwaaminisha wana yanga mambo yapo shwari...wakati lengo lake likiwa ni kujiaminisha kuwa atasolve matatizo ya yanga 100% uwezo huo hana, mtu sahihi na smart wa kuingoza yanga kipindi hiki ni Tarimba au Ridhiwan...wengine ni ujanja ujanja tu, Tarimba kasoma mchezo akaona tatizo...he is very smart...hatoi hela kijinga...
 
Huyu Tarimba aliwahi kupigwa chupa akapasuka juu ya jicho la kushoto Miaka kadhaa iliyopita akiwa Mwenyekiti wa Yanga, nilimshangaa Sana kutamani kurudi pale
 
Shida sio sanga wala Tarimba tatizo ni kwamba hakuna mtu mwenye fedha aliye tayari kuisaidia yanga .. ni propaganda tu ndo zinazoendelea huyo tarimba hajawah kuudhuria kikao chochote alichoitwa na ndugu sanga na wala hajawah kuonyesha jitihada zozote tangu alipoteuliwa na ata katika maelezo yake hakuna sehem aliyoonesha jitihada zozote za kutusaidia..
Tatizo hiv vilabu vya jumuiya havinaga shukran wala subira.. wakat kwenye mkutano mkuu sanga anaomba agenda ya manji isogezwe mpaka itakapo jadiliwa mlisema anampinga manji.. Leo hii kasema ukweli juu ya kukosa ushirikiano toka kwa tarimba mnasema anamtumia manji kuishikiria yanga.. tuwe wenye kusubir na wavumilivu lasivyo hatutofika popote
 
Back
Top Bottom