GE2025 Tarimba anasikitika Wananchi wake kukosa Maji, kama hakuwa Mbunge akijinadi kusimamia Uwajibikaji Kinondoni

GE2025 Tarimba anasikitika Wananchi wake kukosa Maji, kama hakuwa Mbunge akijinadi kusimamia Uwajibikaji Kinondoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni Jijini Dar es asalaam kupitia chama cha mapinduzi CCM Abbas Tarimba amezindua rasmi kampeni za siasa kuelekea uchaguzi mkuu akijinadi kusimamia uwajibikaji endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo kwa muhula mwingine.

Katika mkutano wake wa hadhara ulifanyika katika kata ya Hananasifu, Abbas amenukuliwa akiomba ridhaa ya kuongoza kwa muhula mwingine huku akiomba ushirikiano kwa viongozi wa ngazi ya serikali za mitaa kumaliza kero za wananchi.

Tarimba anawakumbusha wana Kinondoni wajibu aliouchukua kujenga kingo za mto msimbazi na kusimamia vema zoezi la kulipa fidia wananchi waliopitiwa na mradi.

Vyama vya siasa nchini Tanzania vinakoleza moto kunadi sera zao kuelekea uchaguzi mkuu October mwaka huu wakati chama tawala CCM kikisimika kila pahala mgombea wa nafasi zote za udiwani, ubunge na Rais.

 
Back
Top Bottom