Tarime kama Tarime

Tarime kama Tarime

School face

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2019
Posts
247
Reaction score
407
Habari wana Jf,

Moja kwa moja niende kwenye mada tajwa hapo juu. Nimetembelea tarime mjini na vijijini kwa muda sasa lakini nimestaajabishwa kuona kila hotel kubwa au ndogo ya mjini au vijijini.

Unapokua umeagiza msosi unaletewa kwenye sahani za plastic mwanzo niliona kama kitu cha kawaida lakini kadri siku zinavyo songa nikaona hii kitu sio ya kawaida ikabidi niamue kuvunja ukimya nikauliza na hii ni baada ya kwenda kwenye hotel kubwa na kukuta style ileile ya kwenye hotel ndogo ndogo.

Baada ya kuletewa chakula nikabidi niulize ni kwanini hotel kubwa kama hii lakini unaletewa chakula kwenye sahani ya plastic muudumu akaniangalia kisha akanambia wewe ni mgeni nikakubali kisha akaniambia huku kwetu ukiweka sahani za udongo wanazitumia kama siraha pale wanapokua wame pishana kauli kwahyo ndiyo maana tunaweka za plastic huku kwetu ugomvi ni nje nje.

Kwakweli nilishangaa sana kusikia maneno yale haya sasa wakazi wa tarime na viunga vyake ebu kujeni na majibu tosha😂😂😂
 
Back
Top Bottom