tarimemjini
Member
- Jul 10, 2025
- 71
- 142
Baada ya jitihada za CCM Taifa kumbembeleza Ndugu Jackson Kangoye ajitoe kugombea Ubunge Tarime ili kumrahisishia Esther Matiko kushindikana, Tume ya Uchaguzi isiyo huru imeamua kumeungua mgombea huyo.
Esther alimuwekea pingamizi ambalo lilitupiliwa mbali. Na akakata rufaa.
Lakini rufaa ya Jackson Kangoye yenye mashiko imetupiliwa mbali.
Sasa Esther atakuwa mbunge ambaye anapita na kuzomewa na watu hadharani.
=======
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetengua uteuzi na kumuondoa Katika orodha za wagombea, mgombea Ubunge wa jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo Kangoye Jackson Ryoba
Hatua hiyo ya INEC inakuja kufuatia rufaa iliyopokea kutoka kwa mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Matiko Esther Nicholas alyekata rufaa kupinga maamuzi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ambaye alitupiliambali pingamizi lake la awali
Taarifa ya INEC iliyotolewa kwa umma Septemba 03.2025 imeeleza kuwa Tume hiyo ilipokea jumla ya rufaa 51 za kupinga uamuzi wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuhusu pingamizi za uteuzi wa wagombea Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Udiwani kwa Tanzania Bara
INEC imesema katika rufaa hizo 51 iliyozipoke na kuzifanyia maamuzi, rufaa 20 ni za kupinga uamuzi wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuhusu Ubunge, na rufaa 31 ni za kupinga uamuzi kuhusu Udiwani
Kupitia taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzu wa Uchaguzi Ramadhani Kailima imefafanuliwa kuwa miongoni mwa rufaa hizo, rufaa 13 kati ya rufaa 51 zilizotolewa uamuzi katika kikao cha Tume cha Agosti 31.2025 na taarifa yake kutolewa kwa umma siku hiyohiyo
Aidha, INEC katika kikao chake kilichofanyika kuanzia Septemba 01 hadi 03 mwaka huu, imefanya uamuzi wa rufaa 38, ambapo kwa rufaa za Ubunge Tume imezikubali, Tume imezikubali rufaa nne (4), imekataa rufaa saba (7) na kufuta rufaa moja (1), kwa upande wa Udiwani Tume imekubali rufaa tisa (9) na kuzikataa rufaa 17
Kufuatia uamuzi huo, wagombea Ubunge saba (7) walioenguliwa rasmi na hawatokuwa wagombea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni pamoja na Gimbi Dotto Masaba wa CHAUMMA (Itilima), Omary Ahmad Badwel wa CHAUMMA (Bahi), Mohamed Juma Haji wa AAFP (Chambani), Loyce Benjamin Giboma wa CHAUMMA (Ubungo), Pius Ismail Masululi wa ACT Wazalendo (Bunda Mjini), na Kangoye Jackson Ryoba wa ACT Wazalendo (Tarime Mjini),
Chanzo Jambo TV
Soma Esther Matiko amuwekea pingamizi mgombe wa ACT-Wazalendo Tarime Mjini