Mchokozi wa mambo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 201
- 159
Kwakweli inasikitisha kweli kwa kinachofanywa na TARURA katika barabara za Kata ya Kitunda, Mwanagati na maeneo jirani na kata hizo naweza kusema ni uhuni na kutukosea wananchi.
Wameweka bango kubwa la ukarabati wa barabara na kushangaza wamepitisha greda na kumwaga kifusi cha vumbi. Hata kama hatujui huu ni uhuni wa wazi na kutumia fedha zetu za maendeleo vibaya.
Hivi kweli Mbunge wa Ukonga, Madiwani, manispaa pamoja wenyeviti wa serikali za mtaa hamuoni hili linalofanyika?
barabara ya Kitunda- Mwanagati ni vumbi tupu ukipanda pikipiki au usafiri wowote ulio wazi unafikia eneo unaloenda ukiwa kama unafanya kazi mashineni.
Tunaomba wizara na wanaohusika na fedha za ukarabati wa barabara hizi waje wajiridhishe. Hali ni mbaya sana wanafunzi wa shule ya Sekondari Kitunda, Shule ya Msingi Kitunda na Jitihada wanaumia kwa vumbi linalotimuka.
Kitunda kumekuwa kama kichaka cha kupiga hela watendaji na viongozi mbalimbali. Kulikuwa na usafiri wa Magari Mwanagati Mnazi Mmoja na Machinga Complex lakini hivi sasa imebaki historia tu magari yote yanageuzia Kitunda pamoja na yanatakiwa kugeuzia Mwanagati huku trafiki wakiwepo eneo hilo, wanakula rushwa hatuelewi. Sisi wananchi wa Mwanagati kiukweli tunaumia sana kuona magari yetu yapo lakini yanaishia Kitunda.
Pia magari madogo ya Kitunda Banana waliambiwa hii root ife yabaki magari makubwa tu yanayoenda Mjini sasa hatuelewi kwanini mpaka sasa yapo na yanasababisha foleni kubwa ya magari eneo la Njiapanda Msikiti.
Wanaohusika na haya yote fuatilieni mjionee haya.
Asante