TARURA Ilemela Ivunjwe, DED na Mhandisi wa Barabara nao Waondolewe kwa kushindwa kazi

TARURA Ilemela Ivunjwe, DED na Mhandisi wa Barabara nao Waondolewe kwa kushindwa kazi

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
861
Reaction score
2,515
Katika halmashauri za manispaa za hovyo hapa nchini nadhani ile Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Nilikuwa huko kwa mapumziko ya sikukuu na nimejiuliza jee huko TARURA wapo kweli? Na jee Mkurugenzi na mhandisi wake wapo na wanalipwa mishahara?

Hata ukienda juu zaidi jee RC Mtanda naye anafanya kazi ya kukagua maeneo yaliyo ndani ya jiji au yeye yupo kupambania timu ya Pamba tuu?

Nimeshangazwa sana na barabara kubwa kama ya kutokea Pasiansi kuelekea Kiseke PPF kupitia Lumala makaburini kama KM 2 tuu ilivyo chakaa kiasi cha kutopitika kwa baadhi ya magari.

Eneo hili ni la makazi lakini mfano kunatokea ajali ya moto (GOD forbidden) hakuna gari la Fire brigade linaweza kufika kwa wakati labda kwa masaa 24, jee kuna kitu kinaweza okolewa? Hii ilikuwa iwekwe lami na kuna taarifa budget yake ilipita lakini kwa vile madiwani wa Ilemela ni mbumbumbu wao ni biashara ya viwanja tuu basi hawahoji lolote.

Huo ni mfano mmoja tuu lakini Ilemela MC ni kama imeoza tuu na mbunge wake yule ambaye pengine alipewa uwaziri kwa ukabila na hana la maana afanyalo zaidi ya kupiga majungu wenzake.

Waziri TAMISEMI iangalie hii halmashauri na TARURA yake, na naomba waliopo huko kwa sasa watupigie picha a hiyo barabara ili wahusika washtuke basi!

Maana nimesikia siku moja mabasi ya wanafunzi kidogo ya dondoke yalipokuwa yakipishana kwenye daraja lililolika upande.

Vipi hapo walisha jiandaa na kauli "bwana alitoa na alitwaa"?

Timizeni wajibu au ondokeni ofisini
 
Maana nimesikia siku moja mabasi ya wanafunzi kidogo ya dondoke yalipokuwa yakipishana kwenye daraja lililolika upande.

Vipi hapo walisha jiandaa na kauli "bwana alitoa na alitwaa"?
Timizeni wajibu au ondokeni ofisini,🤥🤔🙇🏿‍♂
 
Kipande cha kiseke Lumala ni kipande kidogo sana, yaani kinahitaji maamuzi magumu, tu, labda watakuwa wanaumiza kichwa kwenye lile daraja ambalo lazima walinyanyue liendane na level ya juu ya barabara. Likiwa chini itakuwa shida kwa sababu pale pana maji mengi yanapita.

Otherwise pataondoa msongamano.

Safari ni hatua, na ni alijua kwamba barabara za kirumba-kabuhoro leo zingekuwa vizuri, mpaka kiyungi, na taa za barabarani. Kabuhoro ibanda inachimbuliwa taratibu

Tusubiri lami ya Buswelu Nyamhongolo, nayo inajengwa sasa hivi. The good thing ni mradi wa world Bank, wao kila hatua wanakagua.

Patamu zaidi pale Busenga Cocacola kwenda Buswelu, wasicheze napo kabisa, tutaandamana.

Pia barabara za Sokoni Kirumba zikipigwa mkeka..... Hiiiiiiiii, bhebhe ngosha
 
Uko sahihi, lakini hatua zote za awali zilishafanyika na zabuni ilitangazwa.
Sawa pesa yaweza kuwa imeliwa hasa baada ya mfuatiliaji mkuu Magu kufariki, lakini hata kupitisha greda ili ipitike muda wote wanashindwa?
Ni hatari mjini kuishi eneo ambalo hata gari la zimamoto haliwezi kupita maana mnaweza shuhudia mtaa mzima unawaka na hakuna la kufanya zaidi ya kusema Alhamdulilahi
 
Back
Top Bottom