Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Nikiwa katika eneo la Mtemi Beda Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, nilipokwenda kumjulia hali bibi yangu mzaa baba ambaye ni mgonjwa sana, Nimeona kero ya muda mrefu ya ubovu wa barabara ya Mtaa wa Misukumilo eneo la Mtemi Beda kwenda Kitongoji cha Milala Shongo Kijiji cha Milala.
Nikakumbuka mkataba wa TARURA ya Katavi waliosaini mwezi Novemba, 2024 na mkandarasi moja kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na daraja la Milala Shongo huku sauti ya kiongozi wa TARURA akisema kwamba Milioni 500 zitatumika kujenga barabara na daraja na kukamilika ifikapo Mwenzi wa sita mwaka huu.
Chakushangaza ujenzi pekee uliofanyika ni greda kuchimbua barabara na kuondoka, Sasa najiuliza hizo milioni 500 ndio zimeisha au mkataba ulimtaka mkandarasi kufanya hivyo na kuondoka? au kuna nini kinaendelea? Maana wananchi wanateseka, Hivyo viongozi wenyedhamana chukueni hatua.
==============================
ILIVYOKUWA AWALI...
Wakazi wa kijiji cha Milala kilichopo kata ya Misunkumilo halimashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi inatarajia kuondokana na adhaa iliyodumu kwa miaka mingi ya ukosefu wa daraja linalounganisha wakazi wa maeneo hayo.
Wakazi wa maeneo hayo wameshuhudia mkandarasi akikabidhiwa ujenzi wa mradi wa barabara yenye urefu wa kilomita 13 ambayo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe.
Katika hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusufu amemtaka mkandarasi kuhakikisha anatekeleza mradi huo kulingana na taratibu za mkataba huku akiwasisitizia wananchi wa maeneo hayo kuchangamkia fursa za ajira kupitia mradi huo.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Mpanda, Mhandisi Joseph Kahoza amesema Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 500 ambazo zote zitatumika kutengeneza na kukarabati barabara za maeneo hayo.
Chanzo: The Katavi Independent