Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHA KWA MUDA UTOZAJI WA FAINI ZA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
KUSITISHA KWA MUDA UTOZAJI WA FAINI ZA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
Dodoma 8 Aprili, 2022
Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 07/04/2022 Wakala wa Barabara za Vijijini na MijiniTARURA ilitoa taarifa ya kuanza kutoza faini kwa watumiaji wa maegesho waliopitisha Siku 14 bila kulipa madeni ya Ushuru wa Maegesho kwa madeni ya kuanzia tarehe 01/03/2022.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), baada ya kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maegesho ya Magari kupitia matumizi ya Mfumo wa TeRMIS umeongeza muda wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya Mfumo huu wa kielektroniki.
Kutokana na kuongeza muda wa utoaji elimu kwa wananchi, utozaji wa faini za kuanzia tarehe 01 Machi 2022 unasitishwa kwa muda kuanzia leo tarehe 08/04/2022 mpaka akapoelezwa tena.
TARURA inaendelea kuwasisitza Wananchi kuendelea kulipa ushuru wa Maegesho kwa wakati, yaani ndani ya siku 14 tangu walipotumia Maegesho, kama inavyoelekezwa katika Kanuni za Maegesho, Tangazo la Serikali Na 799 la tarehe 3, Desemba 2021.
Mfumo wa TeRMIS unatoa nafasi ya kupata taarifa za kumbukumbu za madeni ya Ushuru wa Maegesho kupitia Simu zao za mikononi, kupitia Apps za TeRMIS na "GePG zinazopatikana Playstore na Apple Store (kwa GePG pekee)
Aidha, Huduma hii ya Malipo ya Maegesho ya Magari kwa Ki-elektroniki (TERMIS), inapatikana kupitia *152*00#, chagua 4 (Nishati, Madini na Usafiri), chagua 2 (TARURA) halafu chagua 3 (kujisajili), halafu weka namba ya gari lako. ERMIS)
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Wadau waliwahi kuhoji na kushauri