Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa tarura inabidi watoe elimu kwa wenye magari kuhusu hizi kodi za maegesho ili tujue taratibu zao kwenye huu ukusanyaji.TARURA waachane na huu wizi wa mchana kweupe, kama wapo serious wajenge hizo parking ambazo wanataka walipwe..........siyo kuvizia magari ya watu mitaani na kubambikiza tozo. Mbona pale mlimani city watu wanalipia parking bila shida, wao kwa nini wakusanye maeneo ambayo hawajawekeza hadi kwenye maeneo ya watu binafsi wao wanatoza parking. Hivi inaingia akilini, maeneo ya mbele ya biashara za watu TARURA mnatoza parking fee, utadhani hayo maeneo mnayamiliki nyinyi........kwa hiyo ukihitaji kuingia kupata huduma madukani gari tuwe tunabeba mgongoni!!?
Tulia wakunyooshe.Hawa tarura inabidi watoe elimu kwa wenye magari kuhusu hizi kodi za maegesho ili tujue taratibu zao kwenye huu ukusanyaji.
Kwa sasa imekuwa ni kero kubwa sana, nilienda Arusha gari ikapata hitilafu nikaenda gereji maeneo ya Unga ltd, gari imefunguliwa tairi na iko juu ya jeki hawa watu wa parking nikakuta wameniwekea risti ya deni la kuegesha pale. Nilipouliza wahusika wakaniambia ni kawaida kwa hao tarura kuja kutoza pale kila siku.
Gari ni mbovu iko kwa fundi itatozwaje kodi ya kuegesha!?
Kuna shida mahali.
Na kweli hapa tunanyooshwa.Tulia wakunyooshe.
Serikali ya CCM imekosa ubunifu wa vyanzo vya mapato.
Tumeyataka
Tuyanywe
Wamevipanda vingapi na wanaendelea kuvuna ushindi wa kimbunga kila msimu wa mavuno ya uchaguzi?Na kweli hapa tunanyooshwa.
Ila wajue kwamba wanachokipanda watakivuna.