TARURA: Kusitishwa kwa muda kwa faini za ushuru wa maengesho ya magari

Hawa tarura inabidi watoe elimu kwa wenye magari kuhusu hizi kodi za maegesho ili tujue taratibu zao kwenye huu ukusanyaji.

Kwa sasa imekuwa ni kero kubwa sana, nilienda Arusha wiki iliyopita gari likapata hitilafu nikaenda gereji maeneo ya Unga ltd, gari limefunguliwa tairi na liko juu ya jeki hawa watu wa parking nikakuta wameniwekea risti ya deni la kuegesha pale. Nilipouliza wahusika wakaniambia ni kawaida kwa hao tarura kuja kutoza pale kila siku.

Gari ni mbovu liko kwa fundi litatozwaje kodi ya kuegesha!?
Kuna shida mahali.
 
Tulia wakunyooshe.

Serikali ya CCM imekosa ubunifu wa vyanzo vya mapato.
Tumeyataka
Tuyanywe
 
Na kweli hapa tunanyooshwa.
Ila wajue kwamba wanachokipanda watakivuna.
Wamevipanda vingapi na wanaendelea kuvuna ushindi wa kimbunga kila msimu wa mavuno ya uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…