TARURA, suala la ushuru wa maegesho limekua too much!

TARURA, suala la ushuru wa maegesho limekua too much!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu pole na kazi.

Kuna baadhi ya members wamekua wakilalamika kwamba, wakicheki deni la parking ya gari kwenye website ya TARURA, wanakuta madeni ya sehemu ambayo hawajawahi ata kupeleka gari. Wengi tulidhani wanatania au ni mara moja au mbili tu.

Leo kuna mfanyakazi mwenzangu anasema amekamatwa na watu wa TARURA kwasababu ana madeni ya parking, elfu 60. Nikajiuliza kwa parking ya 500 kwa saa, hadi inafika 60,000 ulipark wapi na tokea lini? Nikapotezea.

Sasa nikasema na mimi ngoja nicheki kama nadaiwa. Aisee, nimekutwa nadaiwa 12,000 na list ya parking areas ambazo ata sizijui ni wapi. Serious zote nimebambikiwa sijawahi park ilo eneo.

1719307343754.png

Hawa vijana mnaowapa vishkwambi watembee navyo, nasikia mnawapangia mahesabu, kwamba kila mtu lazima atimize hesabu ya boss. Shida inakuja hawaendi site, wanachofanya wanakaa ndani na kuanza kusuka mkeka. Aisee hii tumefika pabaya.

Tafuteni njia nyingine ya kutunyonya aisee hii mbaya sana, na simu za customer care hampokei, mnakera sana na acheni tamaa za kiwaki. Nawatakia mabaya nyinyi na vizazi vyenu wafanyakazi wote wa hii department, hadi vizazi vya mifugo yenu. Mnatamaa za ajabu sana.
 
Edit:

Nimejaribu kuangalia Gari lenye namba T344EFG ambalo ni very recent, nimekuta lina deni la mwaka 2023, hii namba EFG imetoka miezi michache iliopita lakini mtu anaambiwa ameshapark gari.
Last week nilicheki deni la parking ilikuwa 32,000 na kuna sehemu ambazo hata sizijui inaonyesha nilipark.

Leo hii nimeangalia deni ni 36,000 na inaonyesha baadhi ya sehemu niliyoparki ni Posta.

Cha ajabu gari natumia peke yangu, hakuna mtu mwingine anaitumia. Ninatoka Tabata kwenda maeneo ya Tazara na gari inapaki ndani ya yard mpaka jioni nikirudi nyumbani, hapo ndio najiuliza hiyo 4,000 imekujaje.

Na ukiangalia deni kwa USSD (kutumia dialling code) unakuta deni kiasi kingine, ukiangalia kwa app ya Tarura unakuta kiasi kingine na ukitumumia app ya GePG unakutana kiasi tofauti pia.

Kuna kitu hakipo sawa katika huu mfumo wote wa parking na tusipokuwa makini tutapigwa sana.
 
Mie nmeenda na gari jana posta gari inaangaliwa ina deni la 160k nmeingia benjamin pale ile narud kwenda kuchkua gar naikuta imepigwa cheni.

Kilichoniokoa ni confidence tu walivyoona ile suti na ongea yang wakajua mtu fulani mwsho wakala elf 5 yao ya soda nkachimba.

Sasa nilivyorudi ofisini nikaanza kucheki gari moja baada ya nyingine cha ajabu zote mpka moja tuloisajili last week tumeikuta na deni la 11k wakati haijawahi kutoka hata yard
 
Wakuu acheni ujuaji mwingi. lipeni madeni.

kila mtu ale urefu wa kamba zake. kwani nyie hamkwibi uko maofisini kwenu?

hamjui miezi ya kulipa ada hii? ebhoo!!
 
Wakuu acheni ujuaji mwingi. lipeni madeni.

kila mtu ale urefu wa kamba zake. kwani nyie hamkwibi uko maofisini kwenu?

hamjui miezi ya kulipa ada hii? ebhoo!!
Hamna ambaye amegoma kulipa, cha muhimu tunataka tulipe bills ambazo ni genuine! Sasa unalipa kwa kubambikiwa, mimi nishapewaga bill ya parking gari inaonekana iko ilipaki dar wakati gari iko mbeya na tarehe hizo haikuwahi kuwepo dar!
 
Edit:

Nimejaribu kuangalia Gari lenye namba T344EFG ambalo ni very recent, nimekuta lina deni la mwaka 2023, hii namba EFG imetoka miezi michache iliopita lakini mtu anaambiwa ameshapark gari.
Ndio Tanzania yetu hiyo gari linadaiwa hata kabla halijaagizwa.
 
Last week nilicheki deni la parking ilikuwa 32,000 na kuna sehemu ambazo hata sizijui inaonyesha nilipark.

Leo hii nimeangalia deni ni 36,000 na inaonyesha baadhi ya sehemu niliyoparki ni Posta.

Cha ajabu gari natumia peke yangu, hakuna mtu mwingine anaitumia. Ninatoka Tabata kwenda maeneo ya Tazara na gari inapaki ndani ya yard mpaka jioni nikirudi nyumbani, hapo ndio najiuliza hiyo 4,000 imekujaje.

Na ukiangalia deni kwa USSD (kutumia dialling code) unakuta deni kiasi kingine, ukiangalia kwa app ya Tarura unakuta kiasi kingine na ukitumumia app ya GePG unakutana kiasi tofauti pia.

Kuna kitu hakipo sawa katika huu mfumo wote wa parking na tusipokuwa makini tutapigwa sana.
Yaani hakuna mahala pa kulalamika na huna cha kuwafanya. Hapa ubabe sana
 
Back
Top Bottom