KERO TARURA Tabora karabatini barabara ya Mwinyi, msisubiri mpaka maafa yatokee

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Wanajamvi ngoja nilibwage, Barabara inayotoka Kwenye mataa jirani na Stendi ya Mabasi kuelelekea Uwanja wa Alhasan Mwinyi ni imeharibika kwa kuwa na mashimo jambo ambalo linaleta adha kwa watumiaji

Nimeshuhudia mara kadhaa watumiaji wa ile barabara ambao wengi ni waendesha baiskeli wanaokuwa wamepakia abiria wakiwa wanataka kugongana na waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda sababu ikiwa ni kila mmoja kukwepa mashimo yaliyojaa kwenye ile barabara

Kwa mantiki hiyo Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA wanatakiwa kuifanyia ukarabati ili angalau hiyo kero iondoke au mpaka watu wagongane wafe ndio wachukue hatua? Kwenu wanajamvi.

 
Kweli, hali ya barabara za lami sio nzuri kabisa manispaa ya Tabora. Hiyo hiyo barabara toka kwenye mataa kwenda kuelekea stand ya zamani kupitia pembeni ya restaurant inayoitwa kitu kama ''Chottara restaurant " kama sikosei , yaani ina vumbi na mashimo balaa, cha ajabu hizo ni barabara za katikati ya mji. Kama wapo humu dah basi wachukue hatua haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…