KERO TARURA wilaya ya Kinondoni wananizungusha malipo yangu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, habari ya leo?

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza. Ningependa kujuzwa, hivi raia anapoidai serikali (halmashauri) inachukua muda gani kulipwa stahiki zake?

Ninawadai Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni pesa kwa mradi wao wa Tarura uliopita kiwanjani kwangu. Huu ni mwaka wa 5 sasa tunapelekeshana, kila nikienda ofisini (halmashauri - Magomeni) kutaka kuonana na Mkurugenzi wananizuia na kunipa visingizio vingi tu vya kijinga. Nimeandika barua tatu (3) kwa Mkurugenzi na kuelekezwa mtu wa kuonana naye anisaidie na kutatua suala langu bado nazungushwa tu.

Mh. Mkuu wa Mkoa, tafadhali naomba appointment na wewe maana nahisi ninachezewa mchezo hapa na hela zangu zimeliwa na hawa watumishi wa halmashauri Mkoani mwako. Watumishi wako hawana kabisa ushirikiano, ni waongo mno na hawako pale kufanya kazi bali kuliibia taifa.
 
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, habari ya leo?

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza. Ningependa kujuzwa, hivi raia anapoidai serikali (halmashauri) inachukua muda gani kulipwa stahiki zake?

Ninawadai Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni pesa kwa mradi wao wa Tarura uliopita kiwanjani kwangu. Huu ni mwaka wa 5 sasa tunapelekeshana, kila nikienda ofisini (halmashauri - Magomeni) kutaka kuonana na Mkurugenzi wananizuia na kunipa visingizio vingi tu vya kijinga. Nimeandika barua tatu (3) kwa Mkurugenzi na kuelekezwa mtu wa kuonana naye anisaidie na kutatua suala langu bado nazungushwa tu.

Mh. Mkuu wa Mkoa, tafadhali naomba appointment na wewe maana nahisi ninachezewa mchezo hapa na hela zangu zimeliwa na hawa watumishi wa halmashauri Mkoani mwako. Watumishi wako hawana kabisa ushirikiano, ni waongo mno na hawako pale kufanya kazi bali
weka jina kamili, namba ya simu,,mtaa unakokaa,nyumba namba tukupe msaada wa haraka
 
Back
Top Bottom