TASAC yafuta tozo saba zilizokuwa kero, yawezesha unafuu bandarini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika kipindi cha miaka minne limefanikiwa kufuta tozo saba nyanyaso zilizokuwa ni kero kwa wadau katika sekta ya maji, hivyo kuleta unafuu wa utoaji wa mizigo bandarini.

Mafanikio hayo ya TASAC yametangazwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa TASAC, Nicholous Kinyariri wakati akiwasilisha mada ya Ifahamu TASAC katika warsha ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari.

Mbali na hilo, amesema TASAC imefanikiwa pia kudhibiti nyaraka za mizigo na kuisaidia serikali kukusanya Kodi yake ipasavyo kwa mizigo inayotoka nje ya nchi.

Kulingana na Kinyariri, TASAC, pia imefanikiwa kutoa leseni 804 za kampuni za uwakala wa forodha na leseni 20 za uwakala wa Meli.

Pia Kinyariri amesema katika kipindi hicho Cha miaka Minne wamefanikiwa kutoa gawio la zaidi ya shilingi Bilioni-40 kwa serikali.

Kuhusu changamoto zinazowakabili wamesema ni uelewa Mdogo wa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na TASAC hivyo kuamua kuja na Mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii.
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, hii midude yote inaelea kwenye maji

1621503632461.png
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, hii midude yote inaelea kwenye maji

View attachment 1791610

Hapo ndipo hatuna budi kuwatambua watu makini waliotokea kuishi dunia yetu hii. Kwa mazoea tunaona ni kawaida tu. Lakini vichwa vimetumika.

Fikiria enzi hizo karibia miaka 250 kabla ya kuzaliwa Kristo (246 BC), Mgiriki Archimedes aligundua kanuni kuhusu vitu vinavyoelea na mpangilio wa hesabu zake. Kanuni hiyo (Archimedes principle) ndiyo imewezesha kutengeneza madude kama hayo (mega ships) yanayoweza kuhamisha kijiji kupitia baharini!

Nafikiria angetoa wazo hilo huku kwetu angeonekana mwehu au aliyekosa kazi ya kufanya. Kama yule mwingine aliyeona apple likidondoka chini toka kwenye mti eti “akashangaa”; kwa nini halikudondokea juu au upande?
 
Absolutely!!!
 
Wazungu ni waongo sana
 
"Kuhusu changamoto zinazowakabili wamesema ni uelewa Mdogo wa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na TASAC hivyo kuamua kuja na Mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii."

Hata mimi nina uelewa mdogo kuhusu TASAC. Baada ya kusoma ndiyo nimeona na TASAC inakusanya kodi.

Mwenye uelewa anisaidie utofauti wa majukumu ya TPA na hiyo TASAC.
 
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika kipindi cha miaka minne limefanikiwa kufuta tozo saba nyanyaso zilizokuwa ni kero kwa wadau katika sekta ya maji, hivyo kuleta unafuu wa utoaji wa mizigo bandarini.

Mafanikio hayo ya TASAC yametangazwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa TASAC, Nicholous Kinyariri wakati akiwasilisha mada ya Ifahamu TASAC katika warsha ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari.

Mbali na hilo, amesema TASAC imefanikiwa pia kudhibiti nyaraka za mizigo na kuisaidia serikali kukusanya Kodi yake ipasavyo kwa mizigo inayotoka nje ya nchi.

Kulingana na Kinyariri, TASAC, pia imefanikiwa kutoa leseni 804 za kampuni za uwakala wa forodha na leseni 20 za uwakala wa Meli.

Pia Kinyariri amesema katika kipindi hicho Cha miaka Minne wamefanikiwa kutoa gawio la zaidi ya shilingi Bilioni-40 kwa serikali.

Kuhusu changamoto zinazowakabili wamesema ni uelewa Mdogo wa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na TASAC hivyo kuamua kuja na Mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii.
Uelewa mdogo hata kwa mleta mada ,ni vyema waendelee kutufahamisha TASAC ni kitu gani
 
"Kuhusu changamoto zinazowakabili wamesema ni uelewa Mdogo wa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na TASAC hivyo kuamua kuja na Mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii."

Hata mimi nina uelewa mdogo kuhusu TASAC. Baada ya kusoma ndiyo nimeona na TASAC inakusanya kodi.

Mwenye uelewa anisaidie utofauti wa majukumu ya TPA na hiyo TASAC.
Elewa tu TASAC na TASAF mapacha.
 
TPA ni Mamlaka ya Bandari. Shughuli yake kuu ni upakuaji na ushushaji wa shehena katika meli kupitia bandari zake.

TASAC ni Shirika la uwakala wa Meli, shughuli zake zimegawanyika kwenye Maritime Transport Regulations moja ya kazi zake ni kusaidia perfomance za bandari zetu, Maritime Environment, Safety n Security, hapa inasimamia ubora na usalama wa mazingira ya bahari, maziwa etc. TASAC ni Port State Control kwa maana ni msiajili wa vyombo vya majini vinavyopita kwenye maji yetu. Vyombo vyote vinavyoanzia mita nne kisheria inabidi visajiliwe na TASAC, Pia TASAC wanafanya Shipping Business yaani kufanya biashara ya Meli. Hapa wanafanya Clearing n Forwarding kwenye mizigo yenye maslahi mapana kwa taifa, wanafanya uwakala wa meli maalum, Document control na Ship tallying yaani uhakiki wa shehena.
 
Back
Top Bottom