TASAC yatoa taarifa kuwa Wahanga 17 wameshaokolewa katika ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita

TASAC yatoa taarifa kuwa Wahanga 17 wameshaokolewa katika ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linatoa taarifa kwa Umma kuhusu tukio la kuzama kwa meli iitwayo MV Maman Benita iliyotokea katika Ziwa Tanganyika. Meli hiyo iliyosajiliwa chini ya bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inamilikiwa na kampuni ya Kikongo, iitwayo Établissement Manimani.

Meli hiyo iliyoanza safari yake tarehe 6 Aprili 2024 majira ya saa 12:00 jioni ikitokea bandari ya Kigoma kuelekea Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa imebeba jumla ya abiria 27 wakiwa ni watanzania watano (5), raia wa China wanne (4), raia wa Kongo kumi na sita (16), raia mmoja (1) wa Kenya pamoja na mtoto mdogo.

Meli hiyo iliyotarajiwa kuwasili Kalemie majira ya saa 8:00 usiku, haikufika ambapo asubuhi ya tarehe 7 Aprili 2024, wavuvi walifanikiwa kumwokoa abiria mmoja mwenye asili ya China na kisha kutoa taarifa kwa Mamlaka za Serikali ya Kongo juu ya kuzama kwa meli ya MV Maman Benita katika eneo la Kabimba, nchini Kongo.

Baada ya kupata taarifa hiyo, zoezi la utafutaji na uokoaji lilianza mara moja ambapo hadi kufikia majira ya saa 1:00 usiku wa tarehe 7 April, 2024, wahanga 17 walikuwa wameshaokolewa, kati yao ikijumuisha Wachina 2, Watanzania 3, na Wakongo 12. Aidha, chanzo cha kuzama kwa meli bado hakijajulikana isipokuwa Nahodha wa meli hiyo ameokolewa na timu ya wataalam tayari imekwenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji. Zoezi la utafutaji kuokoa abiria waliosalia linaendelea.

TASAC inaendelea kutoa rai kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo majini kuzingatia Sheria na Kanuni za udhibiti usafiri majini na kuhakikisha chombo kina kuwa na majaketi okozi ya kutosha na kwa vyombo vidogo kuhakikisha abiria wanavaa jaketi okozi wakati wote wa safari ili kujiepusha na maafa yanayoweza kusababishwa na tukio la ajali.

Aidha, TASAC inatoa pole kwa waathirika pamoja na familia kwa ujumla na taarifa kamili juu ya ajali hii itatolewa.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

==============
Taarifa ya awali - Meli ya Maman BENITA yazama ikiwa na abiria 26, aonekana 1 tu

Screenshot 2024-04-08 100233.png

Screenshot 2024-04-08 100200.png
 
Back
Top Bottom