SoC04 TASAF iwe ya kujenga fikra za walengwa kujijenga/ kujikuza kiuchumi na siyo kuwa tegemezi

SoC04 TASAF iwe ya kujenga fikra za walengwa kujijenga/ kujikuza kiuchumi na siyo kuwa tegemezi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Sep 9, 2022
Posts
5
Reaction score
3
Mfuko wa maendeleo ya jamii ulioanzishwa mnamo mwaka 2000 katika moja ya lengo lake lake la kuinua kaya masikini kwa kuwapatia kiasi cha fedha za kujikimu kulingana na mahitaji husika mfano kulipia watoto shule , matibabu n.k Ulikuwa ni mpango wenye nia nzuri na kwa kiasi fulani umesaidia sana baadhi ya familia husika kuweza kujiinua na kujikwamua kimaisha na kiuchumi

Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia sasa hivi wanachama wana uwezo wa kupokea fedha kupitia njia mbalimbali mfano simu za mkononi, benki n.k. Hii imeweza kuwasaidia sana na kupunguza usumbufu wa nenda rudi kwa baadhi ya wanaokaa maeneo yenye mundombinu duni

Katika hali hiyo pia hapo kuna baadhi ya changamoto ambazo zingeboreshwa zingefanya taasisi hii kuwa ya manufaa maradufu zaidi kwa mfano, kufanya malipo direct pale mwanachama/mwakilishi akiwepo na akasainishwa kisha kupewa risiti na kwenda kutoa fedha zake.

Hii ni kwasababu kumekuwa na baadhi ya wanachama kuwa na mahudhurio hafifu huku taarifa zikionyesha wamepokea fedha, hii pia itasaidia kugundua changamoto alizonazo mwanachama mfano,kuumwa, kifo n.k

Kingine ni kuboresha mfumo wa ufuatiliaji kabla ya mtu kuwa mwanachama kwani kumekuwa na baadhi ya kaya kutoweza kusajiliwa kutokana na changamoto kidogo ya namna ya kujieleza ili kukidhi vigezo.

Pia kuwapatia mikopo ya muda mrefu yenye riba nafuu. Kuwapatia fedha na baadhi ya huduma bure haitoshi na haiwezi kuwa suluhisho bali kuwajengea fikra za kujikwamua na kujiendeleza kiuchumi kutoka pale walipo huo ndio msaada mkubwa kwao.

Tasaf isionekane chombo cha kutoa misaada kwa masikini kwani wengi wao hulemaa ni wachache sana hupiga maendeleo kiuchumi. Kabla ya kupatiwa huduma ningependa wafanyiwe usaili kila mwanachama aainishe shughuli ya kiuchumi ambayo anaona ataweza kuifanya ambayo italeta kipato cha kutosha kujikimu na familia yake kisha apewe mkopo kulingana na uhitaji wa mradi au biashara yake huku kukiwa na ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha fedha inatumika kama ilivyopendekezwa naamini baada ya muda fulani kaya nyingi zitakuwa zimejiondoa kabisa kutoka kuwa tegemezi kwa serikali.

Shukraan.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom