Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Wadau wa JamiiForums.com kutoka Moshi Mkoani Kilimanjaro na Kilindi Mkoani Tanga kudai kuwa wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) hawajalipwa malipo yao pamoja na wengine kudai wazee wanatumikishwa kufanya kazi, mamlaka ya TASAF imefafanua.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TASAF Makao Makuu, Zuhura Mdungi amesema:
"Kwanza kabisa TASAF tunatarajia kufungua ukurasa wetu maalum ndani ya JamiiForums.com kwa ajili ya kuwa tunajibu malalamiko na hoja nyingine kadhaa zinazotuhusu badala ya kuwa tunamjibu mtu mmoja mmoja.
“Ni kweli malipo ya Wanufaika yalichelewa na tayari dirisha la malipo imefunguliwa kuanzia Jumatatu hii (Juni 5, 2023) na yanaendelea kwa sehemu zote.
“Kuhusu tuhuma kuwa wanufaika wazee wanafanyishwa kazi ipo hivi, taratibu zetu zinasema wanaotakiwa kufanya kazi ni wale wenye umri wa miaka 18 hadi 65 tu, wengine wenye umri zaidi ya hapo wanaingia katika malipo mengine ambayo yapo katika utaratibu mwingine.
“Suala la kufanya kazi si kwamba wanatumikishwa, ni muundo wa program ulivyo, mfano wanapata ujuzi na wanakuwa pamoja kubadilishana mawazo.
"Malipo ya Serikali yapo tofauti na malipo ya watu binafsi, huwa wanalipwa kila baada ya miezi miwili na TASAF ni taasisi ya Serikali, kuna taratibu zake za kufanya kazi, fedha haiwezi kupotea, hivyo tutafungua ukurasa wetu JamiiForums ili tuwe tunatoa taarifa pindi inapotokea kuna changamoto ya malipo kuchelewa na mambo mengine muhimu.”
================
MALALAMIKO KUHUSU MALIPO KWA WALENGWA
Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TASAF kinapenda kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya walengwa waliofanya kazi katika miradi ya jamii na kucheleweshewa malipo yao. Aidha Kitengo kinatumia fursa hii kuelimisha jamii kuhusu miradi ya ajira za muda na kulipwa ujira. Miradi ya ajira ya muda ni utaratibu wa utekelezaji miradi ya jamii yenye kutumia nguvu kazi, inayoshirikisha walengwa kufanya kazi na kulipwa ujira. Utaratibu huu unafahamika kwa walengwa wote na kabla haujaanza kutekelezwa walengwa huitishwa mkutano na kupewa taarifa za taratibu za miradi hii na taratibu zake.
Miradi inayotekelezwa kupitia ajira za muda inabuniwa na walengwa wenyewe kwa kuangalia mapungufu na kero mbali mbali ambazo zinawakabili. Miradi inayoibuliwa na jamii iko ya aina mbali mbali lakini mingi inahusu upatikanaji wa maji, barabara za vijijini, malambo ya kunyweshea mifugo, hifadhi ya mazingira na masoko
Utaratibu wa utekelezaji wa miradi ya ajira za muda ni kama ifuatavyo:
Tunapenda kutoa taarifa kwamba malipo kwa walengwa yamefunguliwa kuanzia 05/6/2023 na yataendelea kulipwa hadi 19/6/2023 hivyo walengwa wote watalipwa stahili zao ndani ya kipindi hiki. Zoezi hili la malipo linaenda sambamba na kufanya tathmini ya hali za walengwa ili kuwaondoa wale ambao hali zao kiuchumi zimeimarika na hivyo kupoteza vigezo vya kuwemo kwenye Mpango. Kwa taarifa zaidi, tunapatikana kwa simu kwa namba za bure 0800 110057 na 0800 110058 ambazo ziko wazi Jumatatu au Ijumaa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 2.00 usiku.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
TASAF.
Pia soma:
Tanga: Wazee wanufaika wa TASAF wanafanyishwa kazi ndio wanapewa hela. Hivi ndivyo Serikali ilivyoelekeza?
Moshi: Wanufaika wa TASAF wanyimwa malipo yao kwa muda wa miezi mitano, watakiwa kukarabati barabara hadi zikamilike

- Walengwa wanaoruhusiwa kufanya kazi ni watu wenye umri kati ya miaka 18 hadi 65 wasio walemavu, wajawazito au wenye watoto wenye watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili
- Kazi hufanywa na mwakilishi wa kaya, au mwakilishi-mbadala wa kaya
- Utekelezaji wa miradi ya nguvu kazi huchukua miezi 6. Kila mwezi mlengwa anafanya kazi kwa siku kumi tu
- Muda wa kufanya kazi kwa siku ni saa nne. Wakati wa kazi, anakuwepo mtaalam mwelekezi kusimamia utendaji wa kazi
- Malipo kwa kazi hufanyika kila baada ya miezi miwili ambapo mlengwa atalipwa ujira wa siku alizofanya kazi ambazo hazizidi siku 20 kwa kila kipindi cha miezi miwili ya malipo
- Malipo ya walioshiriki utekelezaji hufanyika mara baada ya taarifa zao kuwasilishwa TASAF kwa ajili ya maandalizi ya malipo.