May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kuna wakati utawasikia baadhi ya Wasanii wa Bongo fleva wakifikia hatua ya kuwashutumu wale waliojitokeza na kukaa katikati yao na soko.
Wanachosahau Wasanii wengi ni kuwa kuwa na kipaji ni jambo moja na biashara ni jambo lingine.
Ili kipaji kiwe biashara lazima kuwe na Mfanya biashara. Uwezo au kipaji chako cha kufinyanga Vyungu Kijijini hakukufanyi tu wewe kuwa Milionea, unaweza ukajitutumua kwa kubeba bidhaa zako na kuzipeleka sokoni lakini mara nyingi utaishia kupata hela ya kujikimu tu huku ukipoteza muda mwingi nje ya eneo lako la kazi.
kila shughuli inahitaji "master mind" mmoja au kadhaa mkakaa chini na kugawana kazi, na hivyo kazi yako ikabaki ni kufinyanga tu Vyungu na kupokea pesa.
Kadri yeye anavyonufaika sokoni ndivyo na Mfinyanzi utaneemeka, na huenda sasa akakuwezesha ukanunua vitendea kazi vya kisasa, ukaajiri nguvu kazi zaidi ili kuongeza uzalishaji n.k.
Kati ya changamoto kubwa zinazoikumba tasnia ya Filamu hapa nchini ni kumkosa au kuwakosa hawa Master mind wa kuigeuza tasnia kuwa biashara inayouzika.
Na kwa isivyo bahati hata Mamlaka zikizungumzia tasnia hii zinawaona Wasanii peke yake, na hili ni tatizo kubwa maana tasnia hii imezungukwa na kada mbalimbali na kiukweli Msanii yeye huajiriwa tu kwa "project" iliyopo mezani.
Mpaka pale tasnia itakapompata Mtu au Watu wenye muda na nia njema na jicho la kibiashara kwa tasnia, basi tusitegemee makubwa haswa kwa upande wa tasnia kuwa kibiashara.