Tasnifu za njano5: Kwa jicho la kizalendo, Nyerere alikuwa sahihi kuukanyaga mkataba wa muungano

Tasnifu za njano5: Kwa jicho la kizalendo, Nyerere alikuwa sahihi kuukanyaga mkataba wa muungano

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Kupinga Serikali tatu ni kusaliti Muungano asilia by Mihangwa.

Mara baada ya kusoma makala ya Joseph Mihangwa inayosema "Kupinga kupinga serikali tatu ni kusaliti muungano" sehemu ya kwanza hadi ya nne, nimeona nami nitoe maoni yangu juu ya muundo wa muungano huku nikizingatia "kweli" iliyofafanuliwa na Mihangwa, nimevutiwa sana na uchambuzi wake ulioegemea zaidi "kweli" kuliko mihemko ya ya kisiasa.

Kuongezwa kwa mambo ya muungano toka kumi na moja hadi kufikia ishirini mbili ni ukiukwaji wa mkataba wa muungano na tukizingatia kuwa hao waliongeza mambo hayo hawakuzingatia mkataba wa muungano wakati wakifanya hivyo. Pamoja na hayo, kama lengo lao ni kuelekea serikali moja, basi wako sahihi chini ya ndoto ya umajimui wa Afrika ingawa kisheria na kisiasa wamepotoka.

Huenda mimi sijui maana ya uzalendo, UZALENDO ni kitendo chochote kinachofanywa kwa maslahi ya umma haijalishi hicho kitendo kitakuwa kiko juu ya sheria au chini ya sheria. Sheria na mikataba ya kisheria huundwa na wanadamu kwa kutumia busara na katu sheria na mikataba ya kisheria haijaumba mwanadamu. Hivyo kwa mtazamo wangu ile busara iliyounda sheria ni bora zaidi kuliko hata sheria yenyewe. Mzalendo wakati wa kufanya vitendo vyake vya kizalendo huweza kuonekana ni mvunjaji wa sheria au hata mhaini.

Mfano, serikali ilitaka kununua mitambo ya DOWANS ambayo ni mtumba. Bunge chini ya uongozi wa Mh Samweli Sitta lilikataa kutoa idhini kwa serikali kununua mitambo hiyo. Mh Zitto Kabwe ni moja kati ya wabunge waliotaka bunge liiruhusu serikali ifanye ununuzi lakini alionekana ni msaliti kwa wanaharakiti wa upinzani, na wengine walienda mbele zaidi kwa kusema kuwa Zitto amehongwa. Ni kweli tuko na sheria inayozuia serikali kununua bidhaa mtumba, lakini kwa udharula ule tusingekosa namna ya kutuwezesha kununua mitambo ile pamoja na kwamba tunasheria inayotukataza. Matokeo yake sasa tunailipa DOWNS fedha ambazo tungeweza kuinunua mitambo ile na kuwa yetu, na mbaya zaidi ile mitambo ipo na tunaendelea kuilipia.Tungeweza kuikanyaga sheria hii kwa maslahi ya umma.

Mwalimu Nyerere alivunja vifungu vya mkataba wa muungano huku akiongozwa na nia au haja ya kuunda serikali moja ambayo kwa vyovyote vile inasadifu ndoto ya umajimui wa AFRIKA. Nyerere alifanya yote hayo si kwa maslahi yake na familia yake ya kule Butiama, bali alifanya hivyo kwa lengo la kuona kuwa TANZANIA yenye serikali moja ni mwanzo wa kuzaliwa shirikisho la AFRIKA lenye kuunganisha kanda zote za Afrika kama nchi moja yenye serikali ya shirikisho. Hata Prof Shivi ameikanyaga taaluma yake makusudi ili kuendeleza dhana ya Umajimui wa Afrika, bila shaka hakupenda kuona watanzania wanakwenda kujadili rasimu huku wakiongozwa na dhana halali ya serikali tatu, bali anataka kuwaaminisha watanzania kuwa serikali mbili kwenda moja ndio mpango na habari njema kwa Afrika.

Kosa la Nyerere ni kutumia mabavu katika kutimiza azma yake hii adhimu, angetafuta namna ya kupata ridhaa ya umma wa kitanganyika na kizanzibar katika kuukanyaga mkataba wa muungano, na kwa vyovyote vile ridhaa hiyo ingezaa marekebisho yenye nguvu ya kisheria na kisiasa kwenye mkataba wa asili. Kujitegeza kwa Wazanzibar ni matoke ya viongozi wetu kukiuka mkataba bila kupata ridhaa ya kisiasa toka kwa umma, ridhaa ambayo ndio msingi wa sheria.

Tanganyika na Zanzibar kwa vyovyote vile mipaka na majina yake ni zao la akili za wageni na si wananchi wenyewe wa nchi hizo. Kwanini tusijitengenezee nchi yetu wenyewe? Kwanini tusijivunie nchi tulioitengeneza wenyewe? Kwanini tunashughulishwa na mipaka iliyowekwa na mabepari huko Berlini? Kwanza ni vema umma uelimishwe ni upi muundo sahihi wa muungano, umma lazima upewe na ufundishwe mkataba wa muungano na kisha umma lazima ufundishwe miundo yote ya muungano inayojulikana, na mwisho wenyewe umma utaamua ni nini hasa wanataka.

Pamoja hayo, ukweli utabaki kuwa Serikali tatu ni kiashiria cha ubinafsi na kitu kibaya sana, tuache ubinafsi na tufikirie namna ya kuifanya ndoto ya Nyerere na Kwame Nkruma inatmia. Kuvunja muungano ndio msumari wa mwisho juu ya jeneza ya ndoto adhimu ya Nyerere na Kwame, na kuuboresha muungano kwa kuleta serikali moja ni mwanzo mzuri wa kuifanya ndoto hii inakuwa kweli na yenye kutufaa waAfrika wote bila kuzingatia mipaka iliyowekwa na wakoloni.

Serikali mbili ni mazoea,
Serikali tatu ni ubinfsi,
Serikali moja ndio mpango mwema.

Njano5.
0784845394.
 
Serekali moja ndio mpango,lakini iitwe zantania na makao makuu yawepo zanzbr na kila kitu kuanzia benk na sarafu passport vyote viwepo zanzbr hapo tutaenda sawa.
 
Serekali moja ndio mpango,lakini iitwe zantania na makao makuu yawepo zanzbr na kila kitu kuanzia benk na sarafu passport vyote viwepo zanzbr hapo tutaenda sawa.

ni mwanzo mzuri, mm sioni ubaya wala shaka ya makao makuu ya serikali hiyo kuwa zenj, shaka yangu ni ubinafsi wa wazanzibar.
 
ni mwanzo mzuri, mm sioni ubaya wala shaka ya makao makuu ya serikali hiyo kuwa zenj, shaka yangu ni ubinafsi wa wazanzibar.
hIVI WEWE MTOA HOJA UPO DUNIA gani? unataka ndoto ya kuunganisha africa iwe taifa moja itimie, wakati kuna Boko haram, Al Shabab na muslim brotherhood
ndani ya Africa? Haya ni makundi ambayo yapo kupinga christianisty, sasa usalama wetu wakristo utakuwa wapi? kama hoja yako uliandikia watu waliokufa ili wapumzike kwa amani, basi nakupa hongera, lakini kama uliandikia watu walio hai, ili wateseke na mabomu ya madege jeshi, inabidi ubatizwe na ma baba wa ubatizo hamsini?
 
hIVI WEWE MTOA HOJA UPO DUNIA gani? unataka ndoto ya kuunganisha africa iwe taifa moja itimie, wakati kuna Boko haram, Al Shabab na muslim brotherhood
ndani ya Africa? Haya ni makundi ambayo yapo kupinga christianisty, sasa usalama wetu wakristo utakuwa wapi? kama hoja yako uliandikia watu waliokufa ili wapumzike kwa amani, basi nakupa hongera, lakini kama uliandikia watu walio hai, ili wateseke na mabomu ya madege jeshi, inabidi ubatizwe na ma baba wa ubatizo hamsini?

kaka umeshafika kwenye udini??? kwanini wafikiria usalama wa wakristo na usifikirie usalama wa wanaafrika???
 
Back
Top Bottom