1.Unamteka mtoto wa kike kwa mtutu wa bunduki
2.Kundi la wanaume saba wakatili mnakubali kwenda kumteka, kumdalilisha, kumnyanyasa na kutweza utu wa mwanamke kwa ujira wa fedha?
3.Mnafunga kitambaa usoni mwanamke kisha mnamtoa nyumbani kwake Kibiti mnamsafirisha hadi mapori ya Kisarawe kwenda kumnyanyasa na kumfanyia ukatili
4.Mnajitambulisha kuwa ni maafisa wa chombo cha dola kisha mnatumia gari la kodi za wananchi, pingu na bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu.
5.Mnachana nguo za mwanamke aliyefunzwa kujistiri kwa dini yake safi ya kiislamu tangu utotoni na kumuacha utupu.
6.Mwanamke mmoja anashirikiana na wanaume saba kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa ujira wa pesa tu
7.Mmemaliza kumfanyia ukatili Mwanamke mnamtekeleza maporini mnaondoka na kujiona wajanja... mnajiona mmeyapatia maisha kweli.
8.Nawakumbusha yupo Mungu juu anayeona kila kitu muda wote na sehemu zote. Ipo siku kabla hamjazikwa na kufukiwa na udongo huu mnaotumia kumwaga damu, mtakumbushwa kila tukio moja mlilotenda.
9.Nawaonea huruma ninyi watekaji na wauaji, kwa kuwa najua hamjui watu makatili kama ninyi mwisho wenu unakuwaga vipi.
10.Lakini niwahakikishie akili za upinzani na harakati hazizimwi kwa mtutu wa bunduki na kufuli la Jela tulifikiri mmejifunza kwa Hayati Magufuli
Hamtoweza kuua watu wote,wapo watakaobaki nyuma yetu,wao watatulipia visasi vyetu.hilo mnatakiwa kulielewa siku zote.
Hakunaga Jambo linafanywa na watu zaidi ya wawili likabakia kuwa siri.
Credit: Boni yai Twitter