msumeno
JF-Expert Member
- Aug 3, 2009
- 2,826
- 1,734
Tunafahamiana , tumezoeana na ikitokea akakosekana mtu humu kwa muda mrefu tunaulizana huyu miss chagga mbona hapatikani JF? au waungwana Miss Bantu au MziziMkavu siku hizi hatumuoni humu kulikoni? na kiukweli kabisa tunafahamiana kama ma ghost maana kila mtu ana taswira yake ndio maana tunapokutana kwa bahati mbaya huwa tunabaki kushangaa '' ha! huyu ndio Heaven Sent kweli mbona bonge? ni kwa mfano ukutane na mshana jr akiwa kavaa kama ustadhi au mchungaji si utakataa!! maana taswira uliyonayo kuhusu mshana jnr ni kumuona akiwa na machale na hirizi shingoni au Mzizi mkavu akiwa na tenga la dawa za kisunna. Imagine ukutane na miss changa akiwa kafungasha na guu la bia si utakimbia maana taswira uliyonayo labda ni kuwa na flat screen na miguu miwa!! imagine!!