Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 796
- 918
Habari wanajamvi.
Kwanza kabisa nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa Mungu aliyeiumba nchi yetu Tanzania na akanifanya mimi kuwa miongoni mwa watanzania.
Shukrani za dhati kabisa kwa nafasi ya pili ziende kwa kamati ya maandalizi kwa kunipatia mualiko. Ni jambo la heshima na ufahari mkubwa kwa kijana wa kitanzania kuhudhuria tukio hilo la kielimu.
Pamoja na yote kuwa muhimu, nitoe pongezi za dhati kwa wanazuoni waliowasilisha mada zao pale jukwaani kwa kiwango walichojaaliwa kulingana na muda.
Kwa umuhimu, kabla sijajitosa katika tathmini yangu ambayo ndio dhumuni kuu la andiko hili, naomba nisafishe njia kwa kupita na hoja au ujumbe wa PhD Henry Rodrick.
Aliwasilisha mada iliyobeba jina la : vijana na mitandao ya kijamii. Huku akieleza namna mitandao inavyoweza kuwa na ushawishi kwa vijana, lakini fursa zitokanazo, hatari pamoja na USHIRIKI WENYE TIJA.
Sasa hapa kwenye ushiriki wenye tija, Dr Rodrick amewasihi vijana kuwa na kawaida ya kufanya tathmini binafsi kabla ya kuchapisha maudhui katika mitandao ya kijamii, hii ni ili kuepukana na kile wataalamu wanachokiita STATE COERCION.
Akisisitiza kuwa hata huko nje ambako uhuru wa kuchapisha upo kwa kiwango kikubwa, yapo baadhi ya mambo nyeti kwa dunia yao ukiyachapisha unaweza ukajikuta mikononi mwa vyombo vya dola.
Kwa maana hiyo, naomba sasa nitumie hiki alichokiita DR. Rodrick kama "ushiriki wenye tija", ili kuepukana na state coercion, katika mtandao huu wa JamiiForums, kufanya tathmini laini na binafsi kwa kuangazia mada ile ile ya " kitendawili cha vijana na maendeleo endelevu katika namna ya kuenzi urithi wa hayati baba wa taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.
Sina lengo la kukosoa ! , ingawaje imehamasishwa kitaaluma na hususani katika tukio la kigoda cha leo, lakini niseme tu kuwa : kiu yangu ya kuendelea kushiriki kwa macho na vitendo katika hadhara ile ilipungua baada ya kuona suala la uchumi jumuishi kwa vijana halikuzungumzwa "kinagaubaga".
Katika hadhira ile ya kigoda cha Mwalimu, wanazuoni wetu walipapasa sana na kwa juu juu tu, inawezekana kwa vile kigoda hiki huandaliwa kila mwaka , kwamba, uchumi jumuishi na vijana vilishazungumzwa kwa kina huko miaka ya nyuma.
Ni maoni yangu kuwa, kulingana na hali ya ukosefu wa ajira rasmi na mitaji kudumu kwa takribani miaka kumi na mbili sasa, ni lazima na ni shuruti ya kimkakati kwa kipengele hiki kuelezwa kwa mapana yake. Hatuwezi kuzungumza lugha ya vijana na maendeleo endelevu katika korido za vyuo vikuu huku tukiacha hali halisi na tete inayowakabili vijana mitaani bila kuisemea. Let us move beyond NKRUMAH PRESENTATIONS.
Naomba tukubaliane kuwa, tunapozungumzia neno "kitendawili cha vijana" katika muktadha huu, tutakuwa tunazungumzia mambo kama vile :
Elimu bora
Ajira bora
Afya bora
Usawa katika fursa
Amani
Utu &
Nafasi ya vijana kuamua hatma ya kesho yao.
Asilimia 80 katika haya mambo niliyoyaweka hapo juu yanakwenda sambamba na kipato binafsi cha kijana.
Hayo mambo yote yalizungumzwa katika dira ya Tanzania 2025 . Ingawaje dira 2025 ilitusaidia kuvuka na kuingia kwenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya chini mwaka 2020, miaka mitano kabla ya muda uliopangwa. Haikufanikiwa kikamilifu kwenye upande wa maendeleo ya watu hususani vijana. Ndio maana nataka nizungumze kidogo kuhusu vijana na maendeleo kwa vile hata Mwalimu aliwahi kusema kuwa " ...Development means the development of people, not just objects or buildings..."
Ni lazima tutizame beyond academic papers by confronting the physical realities of Tanzanian youths on the ground.
Kama mmoja wetu angepata nafasi ya kutembelea na kufanya tathmini katika mikoa na wilaya za kiviwanda kama vile Mkoa wa Mwanza na wilaya ya Mkuranga(Pwani). Atajionea macho kwa macho namna hali halisi za vijana zinavyokinzana na mawazo ya Mwalimu Nyerere ya Utu na haki za kijamii.
Wakati dira ya maendeleo ya 2025 ikimaliza muda wake, vijana wamenasa kwenye mzunguko hatari unaochochea umasikini kwa makusudi, mzunguko huu unachochewa na mapungufu mawili ya kimfumo kama ifuatavyo :
1. Exploitation of manual labour / Unyonyaji unaofanyika kwa vijana wanaofanya kazi za vibarua(viwandani).
Katika mkoa wa Mwanza na wilaya ya Mkuranga kwa mfano : wastani wa malipo ya kibarua unaanzia Tsh 5000/= - Tsh 7000/= kwa siku,
No medical care not even formal contracts.
Wengi wao kwa vile hawana namna mbadala basi tayari wameshaanzisha na familia zao. Katika mazingira haya ya malipo kijana atajinasua vipi kutoka katika umasikini ili dira 2050 inapokamilika imkute akiwa gado?
Kwa kipato cha tsh 125000/= - tsh 175000/= kwa mwezi, huyu kijana atalindaje afya yake, mke na mtoto? Ataweza vipi kuilisha familia yake kikamilifu? Atampeleka vipi mtoto wake shuleni achilia mbali nauli za hapa na pale? Atahakikisha vp familia yake inavaa? Atagharamia vp bundle za internet? Hapo ndipo linapozaliwa neno a Youth Question ama kitendawili cha vijana kama ninavyotafsiri.
2. The taxation trap for graduates /Mtego wa kodi kwa wahitimu .
Katika mazingira yaleyale niliyotaja mwanzo, kumbe hata wahitimu wa vyuo vikuu wanaoonekana kuwa na bahati kubwa sana wanapoajiriwa na sekta binafsi (viwandani), kwanza wanaanza na mshahara mdogo sana wa angalau laki tatu. Lakini katika hali ya kuvunja moyo wanakutana na makato ya asilimia kumi na tano ya HESLB, hapo kuna paye, social security, NHIF, mwisho wa siku take home ni angalau tsh 220000/= kwa mwezi.
Katika mpangilio huu wa kijamii, Falsafa ya Education for self reliance ya baba wa taifa imeacha kuwa an instrument of social mobility and has instead become a debt trap.
My Key Argument : Hatuwezi kuzungumza wala kufikia maendeleo endelevu ikiwa kiini cha ukuaji wa viwanda vyetu ni unyonyaji kwa vijana wa kitanzania.
Ndugu Pan Africans, kama kweli tuna nia na heshima kubwa ya kumuenzi hayati baba wa taifa, ni lazima sasa, tuache kubwabwaja na tudai mambo mawili tu ya kimkakati na kimfumo.
1. Usimamizi wa mabavu na thabiti wa sheria za kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi. Ili kukomesha unyonyaji wa kikatili na wa aibu ambapo vijana wanalipwa elfu tano hadi saba kwa siku. Pia iwekwe adhabu kalikwa viwanda vitakavyokiuka utaratibu huo.
2. Marekebisho ya haraka ya mfumo wa urejeshaji wa mikopo ya HESLB. Yatakayofuta mfumo wa asilimia kumi na tano kwa wote hadi mfumo nafuu unaowalinda wahitimu wenye vipato vya chini.
Tusiporekebisha misingi hii ya kiuchumi kwa vijana, kitendawili cha vijana na maendelso endelevu kitabaki kuwa "maneno matupu" na vijana wataendelea kupata taabu katika nchi yao.
SWALI LA MJADALA KUELEKEA DIRA 2050.
Tukitizama hali halisi, serikali yetu inamiliki vyanzo vingi vya mapato. Wakati huo tuna janga kubwa la ukosefu wa ajira tangu mwaka 2014, ambalo limewaacha wahitimu wengi wakiwa na mzigo mzito wa madai ya HESLB. Matarajio ya msingi wa urejeshaji wa mikopo hiyo ni ajira rasmi ambayo haipo !, ni dhahiri kuwa madeni hayo hayalipiki kiasili, lakini pamoja na mkwamo huo, bodi ya mikopo bado inaendelea kutoa mikopo mipya na kuongeza idadi ya wanufaika kila mwaka. Katika muktadha wa taabu hii, Je ! Si wakati mwafaka kwa serikali yetu kufuta au kusamehe madeni yote ya HESLB kwa wahitimu wote ambao wamesugua mtaani katika kipindi hiki cha mass un employment, ili kuwapa fursa ya kuanza maisha mapya na hivyo kuwa chachu ya maendeleo endelevu?
Vijana mnasemaje? Na serikali mnasemaje?
YUSUFU R H SABURA.