Zanzibar 2020 Tathmini fupi mara Baada ya uteuzi wa Dkt Hussein Mwinyi huko NEC ya CCM

Mnyaa kwa kuwa katemwa, tutamchagua kuwa Rais wa JMT baada ya Magufuli.
 
Mimi iki kitu ndio huwa sielewi mgombea wa uraisi zanzibar anapitishwa na nec bara ..kwa nini nec zanzibar wasikae wakapitisha mtu wao huko ndio aje bara wasalimu
Huyo ni mgombea wa CCM, cuf na vyama vingine vinaweza vikampitisha mgombea wao kule kule zenji......
usiwaze...
 
Mimi nilijua Kuna Unguja na Pemba tu.

Kumbe kuna Unguja kusini,Unguja Kaskazini,Unguja Magharibi na Unguja kati.

Mmewabagua wapemba hadi mmeanza kujibagua wenyewe...

Kweli dhambi ya ubaguzi haijawahi kuacha wabaguzi salama.
Yaani kama wanavyobaguliwa wapinzani kule nchi kavu
 
Muungano wetu utakuwa Salama chini ya Dr Hussein Ally Mwinyi
 
Yamechujwa vipi? Walipigia kura wapi hayo majina matano? Kila mtu anajua hayo majina yamepatikana kwa SHINIKIZO kutoka bara. Zanzibar ndio inakufa hivyo, Wazanzibari chukueni hatua haraka.

Zanzibar ife mara 2?
 
Zanzibar ni mkoa tu wa Tanzania. Hizo nyingine ni mbwembwe za kisiasa.
 
Mada kama hizi huwa zinanipa shida sana.

Hubidi nibadili mawani mara tatu ili nisome na kuzielewa, lakini wapi, nabaki na kichwa kinazunguka tu mwisho wa kuzisoma.
 
Jiwe ametambua kwamba anawahitaji wale wazee waliomtangalio kwenye hiko kiti kuliko alivyozani hapo awali, tena hasa kipindi hiki cha uchaguzi, kaona hasara kuna hasara kubwa ya kubaki peke yake, ambayo inaweza kumcost hata kupoteza urais, sasa tayari kashamtega mzee mwinyi, tuone kwa kikwete, je ridhawani atapitishwa kule Bagamoyo? Kwa mkapa atafanyaje? Ngoja tuendelee kutafuna korosho toka mtwara, wakati game linaendelea.
 
Acheni nongwa
Wagombea walikua 31,wamechujwa na kubaki watano
Wagombea ni wazanzibari,wachujaji ni wazanzibari
Dodoma.yameletwa majina ya wazanzibari watano,ni lazima apite mmoja
Acheni nongwa
Mambo ya aibu,mnaifanya Zanzibar koloni la Tanganyika/Tanzania?Mikanganyiko imezidi,unashindwa kuelewa aina hii ya Muungano wetu ni kwa ajili ya nani hasa?Kero zingeisha once and forever endapo kungekuwa na serikali tatu au moja.Hizi mbili,???
 
Mambo ya aibu,mnaifanya Zanzibar koloni la Tanganyika/Tanzania?Mikanganyiko imezidi,unashindwa kuelewa aina hii ya Muungano wetu ni kwa ajili ya nani hasa?Kero zingeisha once and forever endapo kungekuwa na serikali tatu au moja.Hizi mbili,???
Jomba kero zimebakia ngapi unazozijuaa kwani katika hizi serikali mbil
 
Mimi iki kitu ndio huwa sielewi mgombea wa uraisi zanzibar anapitishwa na nec bara ..kwa nini nec zanzibar wasikae wakapitisha mtu wao huko ndio aje bara wasalimu

Ni hilo tu ambalo hulielewi? Mfumo mzima wa muungano haueleweki kabisa. Baraza la wawakilishi na bajeti zao, polisi, uhamiaji, fedha, uraia na mamlaka ya rais ni miongoni mwa issue ambazo hazieleweki kabisa. Halafu kuna hili suali la zanzibar ni nchi au mkoa. Yaani ni rahisi kujibu suali la baina kuku na yai nani kaja mwanzo, kuliko hili la zanzibar ni nchi au mkoa.
 
Hata ukiingia ndani Unguja Kusini kwa mfano, utakuta bado wanabaguana kati ya Makunduchi, Jambiani na Dimbani
Kweli hao watu laana ya ubaguzi inawatafuna Haswaa!
 
Tunaelekea serikali moja tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…