Tathmini Fupi Ya Ligi Kuu Bara Msimu huu

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Simba Wana Nafasi Kubwa Ya Kubeba Ndoo, Nimejarbu Kuziangalia Azam Fc, Yanga Pamoja Na Simba Na Naipa Asilimia 60 Simba Kutwaa Ubingwa Kutokana Na Ubora Wa Kikosi Chao Mwaka Huu, Kama Watacheza Bila Presha Ya Washabiki Wao Au Malalamiko Kwa Timu Zingine Na Wakajidhatiti Katika Kusaka Alama 3 Ndani Ya Uwanja Hakuna Atakayewazuia Kutwaa Ubingwa Msimu Huu, Kwa Upande Wa Yanga Ambayo Mara Nying Hutegemea Zaidi Huwepo Wa Donald Ngoma, Thaban Kamusoko Na Hamisi Tambwe Ili Kupata Matokeo, Hawa Jamaa Wameonyesha Uchovu Wa Hali Ya Juu Hususan Ngoma Ambaye Kaonyesha Hana Kipya Labda Mech Nying Mfululizo Bila Ya Kupumzka Huenda Ikawa Sababu, Juma Abdul Si Yule Wa Mwaka Jana Anashndwa Kabsa Kupush Mashambulizi Huku Cannavaro Na Yondan Licha Ya Kutumika Sana Pia Umri Umewatupa Mkono, Yanga Itategemea Zaidi Performance Ya Mahadhi Ambaye Atleast Amejitahdi Kuonyesha Vitu Msimu Huu, Kwa Upande Wa Azam Fc Bado Kocha Anajenga Timu So Wana Asilimia 10 Ya Kutwaa Taji Msimu Huu
 
mikia ktk ubora wako,yanga haijafungwa hata goli moja sasa hao na Ina magoli yakufunga sita....sasa uchambuzi wako ni kwakuwa mmeifunga mtibwa Jana.?
 
Afadhali umeongea wewe.. Msimu huu hakuna wa kumzuia Mnyama kubeba makombe yote atakayoshiriki.
 
Mimi Simba damu,nakubaliana na wewe 100%....ila uandishi wako utatuponza.
 
Umetoa tathmini nzuri ila imekaa kishabiki zaidi.
 
Tathimini yangu fupi tu, kama hao jamaa uliowaorodhesha hawatakuwa makini,timu za majeshi yetu zitawaumbua.
 
Sikubaliani na uchambuzi wako hasa kwenye viwango vya uwezekano wa Simba kuwa bingwa kufikia 60% wakati Azam umeipa 10%. Unamaanisha Yanga ni 30% Huu ni mzaha mkubwa!

Ukweli ni kwamba uwezekano wa Simba Yanga na Azam kuwa bingwa ni karibu sawasawa! Ukiacha sababu zilezile za msingi kama ubora wa vikosi na wachezaji, ubora wa mabenchi ya ufundi, matuzo safi, na mengineyo yanayofanana na hayo, timu hizi zina ubora uanokaribiana sana. Tofauti yoyote iliyopo au itakayoonekana inatokana zaidi na mambo matatu;

1. Hamu/Njaa ya Ubingwa (40%)
2. Matumizi ya viwanja vya ugenini(35)
3. Ukubwa wa kikosi(25%)

Ukiangalia timu hizi zote tatu, zina ingredients nyingi zinazofanana za kuwa bingwa. Hata hivyo, Azam na Simba zinaonekana kufanya vzr zaidi kwenye vipengele hivyo kuliko Yanga. Kwangu mimi, Simba inaweza kuwa na nafasi lkn kwa utofauti mdogo sana. Simba wana njaa/kiu sana ya ubingwa. Kuanzia mashabiki, wachezaji, viongozi, na wadau wanazungumza lugha moja tu ubingwa. Hili wanalisema waziwazi, tena na tena kila mara. Biblia inasema 'Ajionavyo mtu nafsini, ndivyo alivyo' na Simba tayari wameshajiona wana haki ya kuwa mabingwa, basi 'nguvu hii' itawafikisha mbali sana, kama sio ubingwa basi karibia na ubingwa.



KIPENGELE MCHANGO YANGA AZAM SIMBA
NJAA YA UBINGWA 40% 12% 13% 15%
MATUMIZI YA VIWANJA VYA UGENINI 35% 12.5% 15% 12.5%
UKUBWA WA KIKOSI 25% 13% 13% 14%

JUMLA 37.5% 41% 41.50%
Uwezekano wa nafasi mwisho wa msimu 3 2 1

Huioni hali hii ktk mitaa ya Jangwani kwa sababu tayari wana hangover ya mafanikio ya msimu uliopita. Lugha yao ya mwili inaonesha kujiamini zaidi kwa sababu wanasema ubingwa kwao ni kama kawa. Azam pia inaonekana wana mikakati ya kuda mrefu kupitia benchi lao jipya la kihispaniola, lakini hata wao ukimsikia msemaji wao Jaffary Iddy, muda mwingi ana kauli za 'tunataka kufanya vizuri'. Kitu kizuri kuhusu Azam, pamoja na kuwa na malengo ya muda mrefu, wameanza vizuri ligi, na Wahispaniola wamefit haraka ktk mpira wa kibongo kiasi cha kushinda ugenini mfululizo. Hii ni dalili nzuri kwa timu inaayotaka ubingwa. Tumoena Simba na Yanga zikipata sare ktk michezo yao ya ugenini kwa Ndanda na JKT Ruvu. (Simba wanadaiwa waikuwa ugenini).

Kitendo cha Azam kucheza mara kwa mara kwenye viwanja vya Mabatini na Manungu, kinaweza kuwa kichocheo cha kuzoea mazingira yote kiasi cha kujichukulia pointi huko Sokoine Mbeya. Yanga, hata ile ya mwaka jana ilikuwa ikistrugge sana kupata ushindi kwenye viwanja wanavyoviita chakavu,na tayari wamesikika wakilalamikia uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Simba bado ni pameja kuona watafanyaje wakianza kutoka nje ya Dar, lkn nao huwa na visingizio hivihivi wanapocheza ugenini, mikoani.

Ukiangalia ukubwa kikosi, nashawishika kuipa tena Simba nafasi kubwa. Wana wachezaji wengi wenye ubora unaolingana. Ukiona mtu kama Jjuuko Murshid anasubiri benchi na bado timu inapata ushindi, ujue kuwa mwaka huu Simba wamefanyia kazi mapungufu yao yale ya kutokuwa na wachezaji mbadala. Huu ulikuwa ni ugonjwa mkubwa kwa msimu miwili mitatu huko nyuma ambapo Simba ilikuwa na wachezaji angalau 13 au 14 na wengine wakitajwa kukamilisha tu idadi, tofati na Yanga ambayo aliyeko uwanjani na benhi wote ni ubora mtupu.

Kwa sasa, Yanga wanaoonekana kuwa na pancha kwenye eneo la ulinzi ka kiungo wa ulinzi. Ni ngumu kufikiria kama Yanga inaweza kushinda mechi tatu ngumu mfululizo ambayo Thabani Kamusoko hatakuwepo uwanjani! Eeno la ulinzi nao ni tegemezi sana kwa Vincent Bosou. Kwa upande wa Azam, bado eneo lao la ulinzi halina wachezaji wake fit hususani kaka jambazi, Paschal Wawa. Wachezaji wapya waliosajiliwa bado hawajatuonyesha kitu cha tofauti sana, na badala yake tunaona eneo la ushambuliaji likimtegemea bado John Bocco.

All in all huu ni mtazamo tu na uzuri ni kwamba mchezo wa mpira hautabiriki, maana yake ukidhani hivi kumbe inakuwa hivi.Pia huwa kuna sababu ambazo huwa ziko nje ya upeo wetu mashabiki na wapenzi wa mpira ila kitu kimoja hubaki kuwa kweli kwamba aliyejiandaa vizuri na mwenye ari ya mafanikio hufika mbali katika mashindano. Ni sawa na methali ya Kiswahili isemayo Mgaagaa na Upwa hali wali mkavu.
 
Samahani hicho kijedwali cha takwimu kimegoma kukaa vizuri. Mwenye uwezo wa kukipangilia asidie tafadhali
 
VPL winner prediction 2016/17
Simba 58%
Yanga 22%
Azam 19.5%
zingine 0.5%.
 
Kabla yamashindano yoyote kuanza, wachambuzi huangalia timu shiriki kwenye nyanja zote na kuishia na uwezekano (probability) wa kila timu kutwaa ubingwa. Mambo yanayoangaliwa ni pamoja na ubora wa vikosi, uzoefu, benchi la ufundi, uwezo wa kifedha, historia, n.k. Uwezekano huu mara nyingi huwekwa kwa mfumo wa uwiano (mf. 1/27, yaani kama mashindano hayo yagefanyika mara 27 basi timu hiyo itashinda mara 1. Baada ya hapo hufuatia utabiri utokanao na utendaji (performance) wa kila timu. Lakini sidhani kama mechi nne zinatosha kwa mchambuzi asiye shabiki kutabiri kiufasaha nafasi ya kila timu kutwaa ubingwa. Ni sawa na mkunga kujua jinsia kwa kuangalia sura ya kichanga mara tu kinapochomoza kichwa au hata kwa kukiangalia sura tu!
 
Tathmini au ubashiri?!
Mechi tatu tayari umeshaamua nani atakuwa bingwa katika ligi yenye michezo zaidi ya 20?!
Kama ligi ni mechi tano basi ubashiri wako upo sawa.
 

Una hoja ya msingi lakini tukubaliane kuwa neno "uwezekano" linajieleza vizuri kwamba sio uhalisia. Ni uwezekano tu au probability kama ulivyosema. Wakati mwingine ni vigumu kujua ni muda gani ambao ni sahihi kuwa utabiri unaweza kufanyika na kutoa majibu sahihi. Kuna kipindi wachambuzi hutoa utabiri hata kabla ya mechi moja ya ligi na kweli unakuta inakuwa hivyo, au inakuwa vinginevyo.

Kitu muhimu ni kujua huu ni ubashiri tu, mshindi huwa hapatikani kabla ya ligi la sivyo watu wasingekuwa wanajiandaa.
 
Muda mzuri wa kupata ubashiri wa kutwaa ubingwa ni kumalizika kwa nusu ya kwanza kwa sababu kila timu itakuwa imepata fursa ya kucheza na timu nyengine na kwa hivyo udhaifu na umadhubuti wao utatosheleza kutoa picha ya mwelekeo wao. Muda mzuri kasoro ya huo ni pale kila timu inapokuwa imecheza nyumbani na ugenini.
 
Simba mna ukame wa makombe kwa muda mrefu mithili ya mwanaume ambaye hajajamiiana na mwanamke kwa kipindi kirefu ndiyo maana bashiri zenu zinaonesha kuwa Simba ndiyo itakuwa bingwa.

Yetu macho na masikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…