TATHMINI: Je, hatma ya masomo ya Sayansi ni ipi? Ukizingatia matokeo ya kidato cha Pili na kidato cha nne 2023

TATHMINI: Je, hatma ya masomo ya Sayansi ni ipi? Ukizingatia matokeo ya kidato cha Pili na kidato cha nne 2023

McCollum

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2023
Posts
384
Reaction score
684
Nawapa salamu wanajukwaa, wala tusitumie muda mwingi sana tuingie moja kwa moja kwenye mada tajwa.

Baada ya Baraza la mitihani la Taifa-NECTA kutangaza matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka siku ya leo-29 Jan 2023, nimeona niunganishe na yale matokeo ya kidato cha Pili ambayo yaliwahi kutoka.

Kwa bahati mbaya licha ya kwamba mambo yanaonekana kuwa mazuri, lakini bado safari ya masomo ya Sayansi kwa Tanzania bado ni ngumu. Masomo mama katika Sayansi kama Hisabati, Fizikia, Kemia, Biolojia bado yanaendelea kuwatesa sana wanafunzi. Kuna shule wanafunzi 13 out of 151 ndio waliofaulu somo la Hesabu, tena katika hizo pass 13 pass 9 ni za daraja D.

Kama mdau wa Elimu ya miaka ya sasa, je, unahisi shida ipo wapi? Je, ni wazazi, walimu, wanafunzi au mfumo mzima ambao umeshindwa kuandaa wanafunzi katika ubora wao?

Naomba kuwasilisha
 
Shida IPO Kwa Waalimu wa masomo ya Sayansi!wanashindwa kudeliver materials-huu ndiyo ukweli.

Walimu wa Sayansi wamejaa majivuno tuuu,eti masomo Yao ni ya kiume ndiyo maana watoto wanafeli.
Mwalimu mwenyewe ukimsikiliza atakuambia Sayansi ngumu,mwalimu wa hivi hawezi kumfaulisha mwanafunzi.
 
Vipi upande wa wanafunzi? Wao unaona wapo vizuri?
 
Vipi upande wa wanafunzi? Wao unaona wapo vizuri?
Hakuna mwanafunzi aliye vibaya isipokuwa hawana interest na masomo ya Sayansi,Walimu wa masomo ya Sayansi na Hesabu wameshindwa kuwafanya watoto wawe na interest na masomo hayo.
 
Kutakuwa na mabadiliko ikiwa eneo la elimu kiutendaji halitaingiliwa na mambo ya kisiasa. Mfano kwa sasa hivi kinachopigiwa kelele na jamii nzima ni suala la mwanafunzi kupigwa, ingali kuna suala la kitaaluma eneo ambalo ni muhimu kabisa, zungumzieni taaluma, sababu inayofanya taaluma ishuke ni pamoja utovu wa nidhamu kwa wanafunzi, fuatilia shule zote zenye bendera nyekundu uone hali ya wanafunzi kinidhamu ikoje.
 
Hakuna mwanafunzi aliye vibaya isipokuwa hawana interest na masomo ya Sayansi,Walimu wa masomo ya Sayansi na Hesabu wameshindwa kuwafanya watoto wawe na interest na masomo hayo.
Mwanafunzi kutokuwa na interest hilo kosa linaangukia partly kwa mzazi pia, sasa kama siku zinasonga mzazi yupo tu haelewi mwanae anasoma nini, kitu gani kinamshinda na changamoto kibao hapo ulezi na Elimu vyote vinatupiwa kwa mwalimu.

Juzi tu kuna shule wanafunzi zaidi ya 200 wamepata daraja sifuri tena kwa kidato cha pili, hii ikiwa na maana watarudia na kuongezeka na hawa wanafunzi ambao mwaka huu wameingia kidato cha pili. Sasa kama darasa lina wanafunzi 400+ walimu watajigawa vipi kufundisha na kuwafanya wanafunzi wawe na interest ya masomo? Kila mwanafunzi anatoka nyumbani kwao ambako kuna Jamii, wazazi au walezi ambao kama wange"play" part yao kijana/mwanafunzi angeichukulia Elimu kwa mkazo, kwa bahati mbaya zigo lote wanatupiwa walimu
 
Back
Top Bottom