Ni kweli kuwa elimu ni muhimu sana.
Kama ilivyo kwenye mada, ukiondoa wachache wanufaikao moja kwa moja (na kibinafsi tu) wengine waishabikiao katiba hii ni kwa kutokujua tu!
Katika lundo la wasiojua wamo hasa hawa kutokea awamu ya tano:
Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia. Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi. Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya...
Kwa jinsi walivyo brainwashed kuwasubiri hao kuelewa inaweza kuwa ni rahisi zaidi kuwasubiria wamasai kuukumbatia uvaaji wa suruali.
La msingi ni kuwa mengi yaliyo fyongo na yanayolalamikiwa na wengi yanatokea kutokana na ubovu wa wazi wa katiba iliyopo:
1. Angalia chaguzi zilivyo kosa haki.
2. Angalia utitiri wa viongozi wa serikali wasio na tija wala kuwa na ridhaa ya wananchi.
3. Angalia maamuzi ya uendeshaji nchi yalivyo pokwa toka kwa wananchi na kuwa ni ya kikundi cha watu kwa maslahi yao.
4. Angalia keki ya taifa inavyoliwa na kutembea katika watu na familia zile zile.
5. Angalia vyombo vilivyo paswa kutulinda vilivyo geuka kuwa vya kutukandamiza.
6. Angalia mzigo wa kodi toka kwa watawala wanavyobebeshwa wananchi. Nini uhalali wa Mawaziri, wabunge na wa namna hiyo kutokulipa kodi stahiki ila sisi?
7. Angalia uozo wa kina SABAYA na kuwa waliendelea kuwapo kama majembe kweli kweli ya serikali yetu kwa mujibu wa katiba.
8. Angalia kimuhe muhe kilichompata mama, katiba iliyopo tu ilipowekwa majaribuni.
9. Vipi haya mambo ya ajira? Kwa nini kusiwepo utaratibu mpya wa watu kutokutumikia serikalini na kwenye taasisi zake bila ukomo ili kuhimiza kujiajiri na kutoa nafasi mpya za ajira?
10. Kwa nini wanasiasa wasistaafu sanjari na kada zingine zote?
11. Nk nk.
Tuidai katiba mpya wakati pia elimu ikitolewa. Kwa hakika, hadi hapa wametuchelewesha sana!
Au nasema uongo ndugu zangu?