Tathmini: Kesho bora ya Tanzania inategemea uwepo wa Katiba Mpya

Tathmini: Kesho bora ya Tanzania inategemea uwepo wa Katiba Mpya

Ni kweli kuwa elimu ni muhimu sana.

Kama ilivyo kwenye mada, ukiondoa wachache wanufaikao moja kwa moja (na kibinafsi tu) wengine waishabikiao katiba hii ni kwa kutokujua tu!

Katika lundo la wasiojua wamo hasa hawa kutokea awamu ya tano:

Kwa jinsi walivyo brainwashed kuwasubiri hao kuelewa inaweza kuwa ni rahisi zaidi kuwasubiria wamasai kuukumbatia uvaaji wa suruali.

La msingi ni kuwa mengi yaliyo fyongo na yanayolalamikiwa na wengi yanatokea kutokana na ubovu wa wazi wa katiba iliyopo:

1. Angalia chaguzi zilivyo kosa haki.
2. Angalia utitiri wa viongozi wa serikali wasio na tija wala kuwa na ridhaa ya wananchi.
3. Angalia maamuzi ya uendeshaji nchi yalivyo pokwa toka kwa wananchi na kuwa ni ya kikundi cha watu kwa maslahi yao.
4. Angalia keki ya taifa inavyoliwa na kutembea katika watu na familia zile zile.
5. Angalia vyombo vilivyo paswa kutulinda vilivyo geuka kuwa vya kutukandamiza.
6. Angalia mzigo wa kodi toka kwa watawala wanavyobebeshwa wananchi. Nini uhalali wa Mawaziri, wabunge na wa namna hiyo kutokulipa kodi stahiki ila sisi?
7. Angalia uozo wa kina SABAYA na kuwa waliendelea kuwapo kama majembe kweli kweli ya serikali yetu kwa mujibu wa katiba.
8. Angalia kimuhe muhe kilichompata mama, katiba iliyopo tu ilipowekwa majaribuni.
9. Vipi haya mambo ya ajira? Kwa nini kusiwepo utaratibu mpya wa watu kutokutumikia serikalini na kwenye taasisi zake bila ukomo ili kuhimiza kujiajiri na kutoa nafasi mpya za ajira?
10. Kwa nini wanasiasa wasistaafu sanjari na kada zingine zote?
11. Nk nk.

Tuidai katiba mpya wakati pia elimu ikitolewa. Kwa hakika, hadi hapa wametuchelewesha sana!

Au nasema uongo ndugu zangu?
Mkuu hebu weka mbinu zinazopaswa kufanyika ili kupata katiba mpya. Nadhani nikiona mbinu zako naweza kupata mwanga zaidi.
 
Kwa taarifa yako katiba ni jambo la kisiasa, unawezaje kutenga hisia ama itikadi za kisiasa. Kwa dhati ya moyo wako, ukiacha wanasiasa hasa wa upinzani, ni taasisi gani au mtu mwingine unamuona akidai katiba mpya kwa nguvu zake zote? Hebu tuambie ww, ukiacha hizo itikadi za kisiasa, ni platform gani tunaweza kukutana na kudai hiyo katiba mpya?

Hapa ndipo tunapopotezwa maboya. Tunahitaji uongozi, uratibu na msukumo wa force iliyo na dhamira, uthubutu na iliyo organized.

Chadema, ma Imamu wa Shura na wa namna hiyo tuwapende au tusiwapende, hawa ndiyo watakaotuvusha.

Mzizi mkubwa wa fitina uko hapa:

IMG_20210620_183332_920.jpg

Maimamu wa Shura walifanya haya:

IMG_20210620_101733_140.jpg

Katiba mpya mbona ipo sana hapa!
 
Mkuu hebu weka mbinu zinazopaswa kufanyika ili kupata katiba mpya. Nadhani nikiona mbinu zako naweza kupata mwanga zaidi.

Mkuu japo yote yameelezwa vyema kwenye mada, ninaya summarize tena hapa kwa ufupi kwa ajili yako:

1. Lazima kuwa na uongozi wenye uthubutu kwenye jambo hili. Kuwepo kwa Force yenye nia, dhamira na organization inayoeleweka hakuepukiki. (Chadema, Maimamu wa Shura, na wa namna hiyo wana fit sana hapa)
2. Lazima kuwatambua maadui na washirika vyema. Kujipanga kuvumiliana within limits ni muhimu. Vita hivi vinahitaji watu wanaoweza kuhesabika.
3. Madhara kwa wahanga yanapaswa kufahamika na mipango thabiti ya kuya accommodate ikawepo.
4. Options zote zinapaswa kuwapo mezani. Kupatikana kwa katiba mpya hakuwezi kuja kwa hisani ya wanaonufaika na katiba iliyopo.
5. Elimu itabidi iendelee kutolewa wakati wote wa mpambano. Ni wazi kuwa sote kabisa tu wahanga wa katiba hii japo kwa viwango tofauti tu na wengine kwa kutokujua tu.
6. Pamoja na kuwa Mizani ya ushindi inaegamea zaidi kwetu, tusiache kujifunza na kutumia uzoefu wa wengine na hasa waliofanikiwa katika haraka kama hizi.

Ifahamike jitihada hizi zikishawashwa rasmi upepo utabadilika. Tutegemee top brass toka CCM wakiwamo Mama na wenziwe kujitokeza kutaka kuongoza mchakato huu. Ndipo tume zitakapofuata ambazo nazo tutataka ziwe huru.

Haya ni kama nionavyo miye. Katika hatua hii maboresho kutokea kokote yanakaribishwa. Kwa pamoja tutakwenda mbali zaidi.

Naunga mkono hoja, ila najaribu kuangalia changamoto za utekelezaji wa mapendekezo yako. Tukifanikiwa juu ya nusu ya mapendekezo yako, jambo zuri litatokea.
 
Mabibi na mabwana ni ukweli usiopingika kuwa kesho yetu iliyo bora zaidi inategemea sana uwepo wa katiba mpya. Kwa hali tuliyofikia kunahitajika zaidi mustakabala mpya wa utangamano. Ni wazi kuwa hayupo mmoja ambaye kwa dhati yake asiyekwazika kabisa kwa lolote na katiba iliyopo labda tu, kwa kutokujua au kuwa mnufaika wa moja kwa moja na mapungufu ya katiba hii tuliyo nayo sasa.

Si Mataga, si CCM, si CUF, si ACT, si Chadema nk. Ni chama gani kwa dhati yao wanaishabikia katiba hii kuwa ndiyo mustakabala bora kabisa tunayoistahili?

Si manguli wa siasa wakiwamo kina Bashiru, kina Pole pole, Warioba, Butiku, nk wote hao wangependa uwepo wa katiba nyingine. Wala si hii ambayo ni wazi kuwa wengine katika hawa bila ya kutarajia kwa katiba hii, wamejikuta wakivunjika mioyo ghafla na kweli kweli. Hawakujua kuwa walistahili katiba mpya mapema, lakini sasa wanajua. Jambo la kheri tu.

Kundi pekee linaloishabikia katiba iliyopo kwa dhati (kuacha mambumbu) ni dogo sana na hili ni lile tu linalonufaika madarakani moja kwa moja kibinafsi kutokana na katiba iliyopo. Hawa wala si wengi kuvihimili vishindo vya watakao mabadiliko.

Kizingiti pekee kilichopo kuifikia azma hii inayotakikana na wengi ni kukosekana kwa umoja. Ni vipi Mataga wa CCM na CCM yenyewe iweze kushirikiana na vyama vingine kama Chadema kudai katiba mpya? Hilo haliwezekani japo wote Chadema na CCM wakiwamo Mataga wanaihitaji mno katiba mpya yenye kuwapa wote uhakika zaidi wa kesho.

CCM kushirikiana na wengine kwenye hili, ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Ni wazi kuwa wajinga ndiyo waliwao na ndiyo iliyo hali halisi!

Kupatikana kwa katiba mpya itakayo wanufaisha wote wakiwamo Chadema, kwa msimamo wa CCM ni bora isipatikane tu. Ya kuwa ni heri hali iliyopo iendelee kuliko kwa namna yoyote kuja pia kuwanufaisha Chadema. Ndivyo ilivyo hasa kwa kuzingatia kuwa pamoja na mapungufu yaliyopo, bado pia CCM ndiye aliye mnufaika zaidi.

Anayebakia kwenye harakati hizi za kupata katiba mpya na ya haki, ni Chadema na wachache wengine lakini si CCM. Kwa hali hii upatikanaji wa katiba mpya si rahisi sana, lakini si kuwa eti haiwezekani.

Kunahitajika kujizatiti vilivyo. Kutambua nini kinahitajika, kuwatambua washirika, kuwatambua maadui na kutambua nini cha kufanya kuhusu wote hao na lini.

Hakuna harakati zisizokuwa kuwa na wahanga. Ni muhimu kutambua viwango vyote vya uhanga unaoweza kutokea kutokana na jitihada za namna hii na kuona namna ya kuzi assimilate, accommodate au kuzifidia.

Kwamba litakayemkuta akale tu na wakwao, hiyo si katika zama hizi na kwa niaba na maslahi ya wote!

Hadi hapa tulipo leo, uzoefu uliopo unatosha sana.

Kutegemea kuwa pana mnufaika mmoja mahali kwa utashi wake tu atakuja siku moja akatupa katiba muafaka isiyokuwa na mapendeleo yoyote, haiwezi kuwa option.

Hali kadhalika kutegemea kuwa kwa kudra ya mwenyezi Mungu, siku moja mambo yatabadilika yenyewe ghafla na kuwa sawa, hilo pia haliwezi kuwa option.

Kulielewa tatizo kwa mapana, marefu na kimo chake ni mwanzo mwema wa kulitafutia suluhu ya kudumu.
hivi kwani katiba mpya itawaletea hela? fanyeni kazi achani kelele za kitoto iliyopo inatosha
 
Naunga mkono hoja, ila najaribu kuangalia changamoto za utekelezaji wa mapendekezo yako. Tukifanikiwa juu ya nusu ya mapendekezo yako, jambo zuri litatokea.

Hata hivyo mkuu tambua wala hayako mambo mengi. Kutoka kwenye mada yaliyoko kwenye red yana husika:

IMG_20210621_140854_903.jpg

Ninakazia: "It is not easy, but not impossible."
 
Hata hivyo mkuu tambua wala hayako mambo mengi. Kutoka kwenye mada yaliyoko kwenye red yana husika:

View attachment 1825423

Ninakazia: "It is not easy, but not impossible."

Najua inawezekana, lakini ukiachia cdm na viongozi kadhaa wa kidini, hakuna wengine walio Active kwenye kudai katiba mpya. Wengine wote wanasubiri mchakato ukubalike na wafaidika wa katiba hii mbovu, kisha waanze kujifanya wanatoa ushauri wa katiba nzuri.
 
Mkuu wawepo au wasiwepo wengine "Active kwenye kudai katiba mpya" hii haitakiwi kuwa issue tena.

Wapo ma opportunists wengi kama si wote wanataka kula matunda tu. Hawako tayari kupambana. Kama ilivyo, matokeo ya kwanza ya mapambano yatazaa tume ya kushughulikia katiba itakayo husisha makundi zaidi.

Ma optimists wote wako mkao wa kula. Wanasubiri ipatikane hiyo tume ya kufanyia kazi katiba mpya. Wao hawako tayari kuipigania kupatikana bali wanataka tu kuwapo kwenye tume. Hao huwezi kuwakwepa kabisa.

Namna ya kuyaepuka machungu yao ni kuhakikisha kuwa ule usemi wa kila mchuma janga hula na wakwao umesambaratishwa. Maimamu wa Shura waliliweza hilo.

Si mbaya pia kufahamu mwendazake awamu ya 5 alijipanga na kuwa brainwash vilivyo wenye uelewa mdogo:

Kwa gharama zozote, mwendazake alihakikisha anajipanga na kuwa manipulate wote hao kuwa upande wake.

Hilo ndiyo lile kundi jingine lisilojua uwepi wa mapungufu ya katiba bali lilioaminishwa kuwa wapinzani na kila mwenye nacho ndiyo chanzo cha matatizo yao 😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!
 
Kwa taarifa yako katiba ni jambo la kisiasa, unawezaje kutenga hisia ama itikadi za kisiasa. Kwa dhati ya moyo wako, ukiacha wanasiasa hasa wa upinzani, ni taasisi gani au mtu mwingine unamuona akidai katiba mpya kwa nguvu zake zote? Hebu tuambie ww, ukiacha hizo itikadi za kisiasa, ni platform gani tunaweza kukutana na kudai hiyo katiba mpya?
Ndugu yangu tindo,nakubaliana nawe shingo upande.Natamani tutengeneze Platform itakayoratibu upatikanaji wa Katiba ya Wananchi bila kuhusisha vyama vya siasa simply kwa sababu CCM na serikali yake wakisikia kuwa wawe na uwanja sawa na CDM kwenye mjadala wa Katiba wanachanganyikiwa.Nakumbukia yaliyotokea 2014=kura za maruhani/marehemu na wagonjwa kwa njia ya e-mail.
May be Jukwaa la Katiba.
 
Platform unayoizungumza inaweza kuwa ndiyo hii ninayoiongelea kama tume. Hii kuzaliwa kwake bila kuwapo kwa utashi wa watawala haitawezekana.

Mamlaka inatakiwa kulazimika kuiruhusu platform (au tume) hiyo kuwepo. Vinginevyo hawataikubalia kufanya lolote. Kupata ridhaa ya mamlaka kwenye hilo haitakuwa rahisi na hapa ndipo haswa kwenye ugumu wenyewe tunaouongelea. Kwa hakika, hapo ndipo kwenye ule msingi mzima wa hatimaye kupata katiba mpya.
 
Yawezekana kweli SSH akaweza kuishangaza Dunia kuwa mwanamke wa kwanza Rais wa nchi kuipatia nchi yake KATIBA MPYA !! wacha tuone !!
 
Ndugu yangu tindo,nakubaliana nawe shingo upande.Natamani tutengeneze Platform itakayoratibu upatikanaji wa Katiba ya Wananchi bila kuhusisha vyama vya siasa simply kwa sababu CCM na serikali yake wakisikia kuwa wawe na uwanja sawa na CDM kwenye mjadala wa Katiba wanachanganyikiwa.Nakumbukia yaliyotokea 2014=kura za maruhani/marehemu na wagonjwa kwa njia ya e-mail.
May be Jukwaa la Katiba.

Mkuu mbinu yoyote itakayoleta katiba mpya itumike, ww ukiwa na mbinu yoyote itekeleze bila kusubiri ruhusa ya yoyote, lakini kutaka hivyo vyama vya siasa visiwepo kwenye huo mchakato ni ngumu kidogo, labda kungekuwa na uhakika wa hiyo mbinu yako.
 
Yawezekana kweli SSH akaweza kuishangaza Dunia kuwa mwanamke wa kwanza Rais wa nchi kuipatia nchi yake KATIBA MPYA !! wacha tuone !!

Kumsubiria kwa utashi wake tu, Mama alete katiba mpya itakuwa dhahiri ni kusubiria dodo Kwenye mnazi:

IMG_20210621_152032_417.jpg
 
Ndugu yangu tindo,nakubaliana nawe shingo upande.Natamani tutengeneze Platform itakayoratibu upatikanaji wa Katiba ya Wananchi bila kuhusisha vyama vya siasa simply kwa sababu CCM na serikali yake wakisikia kuwa wawe na uwanja sawa na CDM kwenye mjadala wa Katiba wanachanganyikiwa.Nakumbukia yaliyotokea 2014=kura za maruhani/marehemu na wagonjwa kwa njia ya e-mail.
May be Jukwaa la Katiba.

Au mkuu hii platform unayopendekeza kwa mawazo yako inazaliwa vipi? Au tufanye je kuipata?
 
China hawajui demokrasia, lakini ndiyo imepiga maendeleo kiuchumi kuliko nchi zote duniani kwa miaka 30 iliyopita . Maendeleo yanaletwa na nidhamu ya kutumia fedha kwa matumizi sahihi yaliyopangwa na nidhamu ya haki ya juu kiutendaji. Siwezi kubeza umuhimu wa Katiba mpya , lakini peke yake sio kitu cha kuleta maendeleo
 
Mkuu usiishie China tu, hata North Korea, Iran, Saudia, nk kuliko na inayoitwa mikono ya chuma na kusemekana kuna maendeleo.

Waulize Ethiopia, Rwanda au hata Tanzania awamu ya Tano. Kwani makelele yote haya ya nini? Hatutaki tena nchi kuendeshwa kama shamba la mtu.

Panga pangua hakuna kilicho bora kuliko demokrasia. Ulizia Bangladesh, Kenya, SA au India pamoja na umasikini wao.

Serikali kama ni watu waache watu wenyewe wajitawale kwa ridhaa zao si kwa utashi wa mtu.
 
Nakubaliana nawe kuwa CHADEMA wanabeba dhima kubwa kwa sababu ya dhamira yao ya msingi ya Democracy.Ila tatizo ni propaganda za CCM kwamba Wananchi hawahitaji Katiba Bali maendeleo ambayo hata hivyo hayaonekani kwa sababu ya Katiba mbovu.
CCM wanatumia vitisho kuwahadaa Watanzania kwamba wanaodai Katiba ni wabinafsi.Wanawazubaisha Wananchi kwenye kuzindua madaraja na makongamano&fiesta.Kila shughuli ya kitaifa wanavaa jezi zao na kuburudika na singeli za kina Zuchu bila kuwapa Wananchi fursa ya elimu ya uraia.
Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama.
Unataka iwepo kura ya maoni kabla ya kupatikana Katiba Mpya? ukiiruhusu hiyo CCM watachakachua, coz wanazo weapon za kila aina kufanya hivyo.

Usiogope kelele za CCM kwenye hili, hata wao CCM wanajua Katiba Mpya inahitajika kila pembe ya nchi yetu, JK kufanya kile alichofanya hakupenda, ilimlazimu kufanya vile, naamini tukifanya kwa Samia pia itawezekana.

Hili lazima lifanyike bila kujali uwepo wa "snitch" kama viongozi wengine wa vyama vya upinzani, wacha Chadema ianzishe, then viongozi wa makundi mengine kama dini, taasisi za kiraia, na wengine wataunga mkono pale watakapoona matokeo chanya ya movement.

CCM wajanja, wanataka hili liachwe kwa vyama vya upinzani pekee mathalan Chadema ili iwe rahisi kwao kusema wananchi hawako tayari, na pale ambapo viongozi wa dini kwa mfano wakianzisha wataambiwa msichanganye dini na siasa, hii game wacha Chadema waiongoze wengine watafuata.
 
Tayari kinaumana. Tarehe 1 July ni rasmi:

IMG_20210621_194913_907.jpg

Cha kujizatiti - Kamanda Muliro anaweza kumbuka kama Mambosasa na kama Muroto.

Mikakati inatakiwa kuwa imewekwa tayari. What if?

Hapa ndipo kwenye kuwapa salamu ya vipi tumedhamiria. Wasaa muhimu sana.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom