Majibu wanayafahamu mioyoni mwao ila hadharani watakueleza mambo aliyofanya Rais,mafanikio ya Serikali za Mitaa ndiyo hayo hayo anayosemewa Mh.Magufuli.Hakuna majibu tofauti,wananchi bado wananyanyasika na kubaguliwa kupata huduma muhimu za kijamii kwa sababu ya Itikadi zao na Rushwa iliyokithiri karibu kila kona.Traffic bado wanakusanya faini kubwa kwa wale wasiotoa elfu 2000-5000 za kupigia viatu Brush/Rangi/KIWI kuanzia yule wa barabarani(Torch),OCS,OCD,RPC hadi Juu mgawo unafikishwa ipasavyo.Ukitaka kuamini haya niyasemayo,tembelea Barrier zote Tanzania uangalie magari yanayofikishwa vituoni kwa makosa ya barabarani mengi ni ya ajali ila ubovu na ukiukwaji wa sheria zingine Traffic wanahukumu field huko huko.Hali ipo hivyo kwa sekta zote.
Sasa Watanzania wakikubali tu matokeo kama ya SM katika Uchaguzi huu Mkuu,Tumejiingiza kichinjioni na hivyo hatutakuwa na pa kukimbilia.Hatari ni kubwa kuliko tunavyofikiri.