Ni wazi kuwa kama nchi tunapita wakati mgumu sana uliohitaji busara zaidi kuliko maguvu.
Kuna shida ya maji Dar tuliyoaminishwa kuwa ni kupungua kwa maji mto Ruvu japo unaendelea kumwaga yake baharini.
Hivi kiwiano, maji kiasi gani yanavunwa Ruvu kulinganisha na yanayoishia baharini?
Kwamba leo tunaanza kulaumu hata ng'ombe kunywa maji ruvu na kilimo cha umwagiliaji?
Kwani huko kanda ya ziwa ambako shida ya maji nako imekamata kama Dar tu, nako ziwa Victoria limekauka?
Tusipoangalia tutamlaumu sana dobi na hata kutupia makombati juu, lakini kaniki litaendelea kuwa na rangi yake.
Faulo inazocheza serikali dhidi ya watu wake isijidanganye kuwa hazionekani. Ifahamike wapo watanzania wengi tu wasioridhika na faulo hizi waliomo ndani ya serikali yenyewe.
Kwamba watanzania hawajui madege mnayonunua kwa pesa zetu msizokuwa na mchango wowote, hatuzihitaji?
Kwamba watanzania hawajui faulo mnazofanya mahakamani?
Kwamba watanzania hawajui faulo mnazofanya bungeni?
Kwamba watanzania hawajui faulo mnazofanya polisi?
Kwamba watanzania hawajui faulo mnazofanya kwenye taasisi ipi? Kwani mnadhani wote ni wafuasi wenu?
Hamukuwahi kusikia viwalavyo vi nguoni mwenu?
-----------
Serikali ni kikundi cha watu kilichojitwalia madaraka kutoka kwa wananchi