Tathmini ya Corona: Wananchi wanachukua tahadhari

Tathmini ya Corona: Wananchi wanachukua tahadhari

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana hii ni tathmini fupi ya matukio yanayoendelea na ugonjwa huu hapa nchini. Kwa hakika ni wazi kuwa pana tafahadhari nyingi na za msingi sana ambazo sasa hivi wananchi wao kama juhudi binafsi tu, wanazichukua.

Ama kweli "Mwenye macho haambiwi tazama." Kama vifaranga wa kuku sasa hivi watanzania wanachakura vilivyo labda baada ya kutambua kumsubiria mama kuwafunza wanachelewa bure.

Ninaleta uzi huu baada ya kuwa nimeshiriki katika shughuli za mazishi kadhaa zikiwamo kuwasafirisha wapendwa kadhaa waliotangulia; kwa mazishi ndani na nje ya Dar.

Kwa hakika wananchi wanaonekana kuwa wamefuzu kwa mafunzo ya vitendo. Wananchi wamepigika na wametambua kuwa ni lazima kubadilika.

Kwa hakika aisifuye mvua, si bure! Baada ya mama kutowafunza, kwa hakika dunia imewafundisha bahati mbaya kwa hesabu za wafu!

Yafuatayo ni niliyoyaona:

1. Kuna mwamko mkubwa sana wa kuvaa barakoa kwa waombolezaji kwa Dar kuliko mno kulinganisha na huko mikoani.

Ni wazi kuwa kwa siku za karibuni kwenye mikusanyiko ya mazishi Dar waombolezaji waliovaa barakoa ni wengi zaidi kuliko wasiovaa.

Kimsingi si nadra kuona hata kufikia 95% ya waombolezaji wakiwa wamevaa barakoa kwenye msiba mmoja.

Jambo la kheri kabisa.

2. Heshima za mwisho Dar kwa marehemu wengi kwa siku za karibuni, zinatolewa sasa bila ya kufungua majeneza tena, kulinganisha na ilivyo kuwa siku za nyuma.

Hii ni mahsusi zaidi kwa wale wapendwa wengi wanaokuwa wametangulia, changamoto za kupumua zikiwa sehemu ya visababishi.

Jambo la kheri kabisa.

3. Katika moja ya misiba, kigogo mmoja wa serikali alikataa kutumia microphone iliyokuwa ikitumika kwenye matangazo mbali mbali hapo msibani.

Mnene huyo alichagua kutoa neno lake bila ya kujali kuwa kusikika kwake kulikuwa kwa taabu katika kadamnasi hiyo.

Jambo la kheri kabisa.

4. Uwepo wa watu msibani umekuwa unazingatia sana kupunguza mrundikano. Primitive social distancing inakuwa implemented na wananchi kama juhudi binafsi.

Jambo la kheri kabisa.

Jitihada zinazofanyika kuwaelimisha wananchi pamoja na vizingiti vilivyopo hazipotei bure.

Alisema Museveni, "maendeleo ya Uganda hayawezi kuwasubiria wakaramoja kujua umuhimu wa kuvaa suruali."

Kitisho cha ugonjwa huu ni dhahiri.

Watu wanapoendelea kufa, bila kujali nani anasema nini, mwenye macho haambiwi tazama. Wananchi waendelee kuchukua hatua.

Penye nia pana njia.

Ninawasilisha.
 
Hata wapiga zumari na mapambio hii Leo pambio na zumari zinaanza kuchukua mwelekeo tofauti.
 
Kuna mambo muhimu ya hekima ya kutambua nyakati hizi:

1) Ni jambo la heri kumsindikiza mwenzetu katika safari yake ya mwisho, pale mmoja wetu anapokuwa ametutoka lakini ukweli ni kuwa hata tumzike tukiwa wengi kiasi gani, hatuwezi kumrudisha wala kumwondolea umauti. Ushauri ni kuwa watu wote wenye umri zaidi ya miaka 45 wasihudhurie mikusanyiko ya misiba. Kama ni lazima sana, mathalani ni ndugu wahusika wakuu, utaratibu maalum uwe umeandaliwa wa kuwakinga kwa namna ambayo inawapa hakikisho kamili la kutopata maambukizi.

2) Kwenye msiba, hatari kubwa iliyopo siyo marehemu aliyefariki kwa covid 19 bali ni ule mkusanyiko. Hivyo tahadhari ya corona kwenye mkusanyiko wa msiba haitegemei marehemu amefariki kutokana na tatizo la corona au tatizo jingine.

3) Msiba unapotokea, wanafamilia wanakuwa wamepoteza control ya kufikiria jambo lolote zaidi ya mpendwa waliyempoteza. Watu hawa ni rahisi sana kupata maambukizi kutokana na watu wengi wanaotaka kuwapa pole. Ni vema mara msiba unapotokea, msiba uliosababishwa na kiti chochote, wafiwa walindwe, wawekwe sehemu ambayo hawafikiwi moja kwa moja na wanaokuja kuwafariji. Kutokuwepo kwa ulinzi wa wafiwa, imekuwa ni sababu ya ongezeko la vifo ndani ya familia ambazo zilipata misiba mingine awali

4) Epuka mikusanyiko, bila ya kujali ni mkusanyiko wa kitu gani. Mikusanyiko mikubwa inayofahamika ni mikusanyiko ya misiba, sherehe, ibada na mikutano.

5) Jitenge kadiri uwezavyo kukutana na watu ambao unafahamu walikuwa kwenye mikusanyiko. Unaweza usiende kwenye mikusanyiko. Rafiki yako au ndugu yako akawa ameenda. Ukikutana naye huyo, ni sawa na wewe ulikuwa umeenda. Na wewe uliyeshiriki kwenye mikisanyiko, ukitoka huko usipende kukutana na watu wengine mpaka kwanza angalao zipite siku 14.
 
Kuna mambo muhimu ya hekima ya kutambua nyakati hizi:

1) Ni jambo la heri kumsindikiza mwenzetu katika safari yake ya mwisho, pale mmoja wetu anapokuwa ametutoka lakini ukweli ni kuwa hata tumzike tukiwa wengi kiasi gani, hatuwezi kumrudisha wala kumwondolea umauti. Ushauri ni kuwa watu wote wenye umri zaidi ya miaka 45 wasihudhurie mikusanyiko ya misiba. Kama ni lazima sana, mathalani ni ndugu wahusika wakuu, utaratibu maalum uwe umeandaliwa wa kuwakinga kwa namna ambayo inawapa hakikisho kamili la kutopata maambukizi...

Ulichoandika ndiyo ulio ukweli mchungu ambao ni vyema watu wakafahamishwa badala ya kuwasubiria kujifunza wenyewe (the hard way) kwa kupitia uhesabu wa vifo.
 
Back
Top Bottom