MANAKE MKARI
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 299
- 240
Kwa kweli tuache mada za kulima kwenye vitabu. Mimi nina uzoefu wa kutosha katika kilimo hiki cha machungwa . Mbegu ambayo iko sokoni kwa sasa ni valencia na kama umejitahidi sana kuzaa ni Machungwa 1500 tena baada ya miaka 4 au 5 huo ndio uhalisia
Mbegu hiyo sina uzoefu nayoMkuu unauzoefu na matombo sweet?Uzaaji wake ukoje?
Lengo lako ni kuuza miche, ili upate wateja wengi umeamua utudanganye idadi ya machungwa kwa mche.mm nina uhakika na niliyokwambia kua mche mmoja unazaa mpaka 4000 na isipokua wakulima waliowengi hata hao wanaopanda valencia hawafuati masharti ya kilimo cha machungwa michungwa ya aina ninayokwambia ni kwamba inauwezo wa kuzaliasha 4000 ikiwa utafuata masharti niliyokueleza katika gharama hasa katika umwagiliziaji
Hello nilikua naomba msaada wa jinsi ya kupanda Haya machungwajamani acheni uswahili anaetaka kuona marejesho nimesema afike shambani
Mtoa mada amechukuli wasimaji wake wana basic knowldge ya kilimo hivyo hakuingia kwa undani. Ila kwa mwenye abc ya akilimo anaelewa. Badala ya kumuuliza maswali suspicious ni vizuri kuwa positive kwani atatoa majibu kadiri ya mahitaji. Kwa mavuno ya 4000 kwa mti, maana yake hii ni aina iliyoboreshwa. Hili hakulisema ila lipo wazi. Na kwa mavuno ya miaka mitatu ina maana ni mchungwa ulio fanyiwa budding. Na kwa miche 76 kwa eka ina maana unapanda mita 8.7x8.7m kati ya mche na mche na mstari. Nadhani hii ni kwa sababu mti wake unakuwa na umbo kubwa kwani michungwa ya kawaida hupandwa kwa 5x5m kawaida. Ni vizuri tukamfuatlia na kuwa positive kwa wenye interest na somo hili. Naona fursa hapaNaulizia kuhusu hiyo mbegu. Je unafanya grafting ili kupata mbegu bora yenye kuchukua muda mfupi mpaka kuzaa matunda?
Mkuu kama ukachimba kisima, ukawa na maji mengi na michungwa yako ukamwagilia kwa irrigation ya drip line, michungwa itazaa mara ngapi kwa mwakaMimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.
Machungwa yanaenda kwa msimu na huwa yanazaa mara mbili kwa mwaka tu hiyo ya irrigation sijaiona ikitumika mahali popoteMkuu kama ukachimba kisima, ukawa na maji mengi na michungwa yako ukamwagilia kwa irrigation ya drip line, michungwa itazaa mara ngapi kwa mwaka
Sent using Jamii Forums mobile app