Swahili_Patriot
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 358
- 831
Tz ni kubwa sasa.Tangia corona ianze mpaka imeisha sijawai kuona mtu yeyote anaeugua corona,japo sio sababu kwamba corona haipo,ipo ila sio kiviile kama mabwege wa mitandaoni wanavyojaribu kuikuza.
I was sick but nime fukizaaaaa weee sa hiv nadunda mitaani.Binamu yangu ni mtu mzima sana pale Dodoma Makole Dodoma, ni mtu mzima, umri wake ni mkubwa na anaugua BP, Kisukari na tezi dume, bahati mbaya akapana na Corona, tulishajiandaa kwa mazishi, huwezi amini amepona na familia yake yote imemaliza kipindi cha karantini wapi safi wote.
Serikali ya Tanzania ilijipanga vilivyo mapema sana kupambana na kuenea kwa Corona. Mwanzo kabisa tulidhibiti mipaka yetu na kuwaweka katika "Isolation centres" kwa muda wa siku 14 kwa yeyote aliyeingia nchini(Kumbuka Diamond na kundi la WCB), na tulifanya "contact tracing & Isolation" kwa nguvu sana pale mwanzoni kabisa kabla haujasambaa sana.Huu uzi unaonyesha wazi kwamba kunao wale wasioamini kuwa kipo na kuna walioadhirika binafsi au familia na marafiki.
Ivi ni ratiba/tahadhari gani unayostahili kuifuata, aidha kuepuka corona au kupunguza kueneza...na ni lipi serikali inafanya kulingana na hio...
Huko Kunyaland mnagonga 10,000 infections wiki hii!Corona yenyewe ipo, na wengi wanaumwa kimya kimya, huku Kenya pia huo ndio mwendo, kuna wale wanapambana nayo kitaani bila kujitokeza, ila tatizo kubwa la mbinu za kihivyo ni pale unagoma kwenda kupimwa kisha unaambukiza mtu asiye na kinga bora mwilini, kunao watu wa kisukari, HIV, msukumo wa damu n.k.
Hamna jinsi unaweza kuwalinda hao kwa kujificha na kirusi cha corona kwako, muhimu upimwe pale unahisi dalili kisha jifungie karantini ili kuwalinda uwapendao.
Mimi hapa kwangu kila siku mwendo wa malimau na maji moto, nimesubiri sana hicho kirusi tupishane kwa amani ili nipate kinga dhidi yake kwa siku za usoni, yaani herd immunity, ila huwa naona kuna namna hakipo tayari kukabiliana na mimi kwa sasa.
Nashukuru sana serikali yetu kwa kuendelea kupima na pia mikakati yote inayofanya haswa kwenye kuskliza wataalam bila kuingiza siasa, sisi hatupo kwenye kampeni hivyo kwa sasa kitu kama hiki hatuwezi kukicheza kisiasa. Ifahamike imbeainika kikubwa kinachotuokoa Afrika ni zile chanjo za homa ya njano, kwamba mataifa mengi ambayo hutoa hizo chanjo hawafi sana licha ya kuathirika.
Halafu wazungu kwao huko hawawezi haya mambo ya herd immunity maana wana wazee wengi sana hususan mijini, sio kama sisi Afrika hapa life expectancy yetu ni ndogo, kwenye miaka 60 huwa tunaanza kujifia mapema, wengine wanarudi vijijini.
Weka vyeti vya kifo hapa... hatutaki porojo za kisiasa!Tz ni kubwa sasa.
Mi nimepata mkosi wa kufiwa na ndugu mmoja na marafiki wawili kwa corona.
Dem wangu na marafiki zake walili waliugua corona na wakapona.
FB friend mmoja aliniconfirmia mwenyewe kuwa alipokuwa kimya alikuwa anapigania uhai kwasababu ya corona.
So mimi binafsi corona imenigusa sanaa.
Mimi si mwanasiasa mdogo wangu, document unazozitaja siwezi zileta kama unavyotaka. Kama hauamini- inatosha kuwa upande wa wasiyoamini na maisha yaendelee.Weka vyeti vya kifo hapa... hatutaki porojo za kisiasa!
Uambatanishe na ripoti ya daktari!
Kwanini hutaki kukubaliana na ukweli kwamba Tanzania Corona imepungua sana ukilinganisha na nchi zingine?. Hivi Kenya mnaweza kuthubutu kufungua vyuo na shule zote bila wanafunzi kuambukizwa kwa wingi kiasi cha wazazi kuwarudisha watoto wa majumbani?.Corona yenyewe ipo, na wengi wanaumwa kimya kimya, huku Kenya pia huo ndio mwendo, kuna wale wanapambana nayo kitaani bila kujitokeza, ila tatizo kubwa la mbinu za kihivyo ni pale unagoma kwenda kupimwa kisha unaambukiza mtu asiye na kinga bora mwilini, kunao watu wa kisukari, HIV, msukumo wa damu n.k.
Hamna jinsi unaweza kuwalinda hao kwa kujificha na kirusi cha corona kwako, muhimu upimwe pale unahisi dalili kisha jifungie karantini ili kuwalinda uwapendao.
Mimi hapa kwangu kila siku mwendo wa malimau na maji moto, nimesubiri sana hicho kirusi tupishane kwa amani ili nipate kinga dhidi yake kwa siku za usoni, yaani herd immunity, ila huwa naona kuna namna hakipo tayari kukabiliana na mimi kwa sasa.
Nashukuru sana serikali yetu kwa kuendelea kupima na pia mikakati yote inayofanya haswa kwenye kuskliza wataalam bila kuingiza siasa, sisi hatupo kwenye kampeni hivyo kwa sasa kitu kama hiki hatuwezi kukicheza kisiasa. Ifahamike imbeainika kikubwa kinachotuokoa Afrika ni zile chanjo za homa ya njano, kwamba mataifa mengi ambayo hutoa hizo chanjo hawafi sana licha ya kuathirika.
Halafu wazungu kwao huko hawawezi haya mambo ya herd immunity maana wana wazee wengi sana hususan mijini, sio kama sisi Afrika hapa life expectancy yetu ni ndogo, kwenye miaka 60 huwa tunaanza kujifia mapema, wengine wanarudi vijijini.
Kwanini hutaki kukubaliana na ukweli kwamba Tanzania Corona imepungua sana ukilinganisha na nchi zingine?. Hivi Kenya mnaweza kuthubutu kufungua vyuo na shule zote bila wanafunzi kuambukizwa kwa wingi kiasi cha wazazi kuwarudisha watoto wa majumbani?.
UNICEF wenyewe wamekiri na kusema ni salama kwa wanafunzi kurudi mashuleni, wewe unayeendelea kukataa na kubisha unalengo gani?.
Utajipimia kila mtu hata kama hana dalili wala historia ya kukutana na mgonjwa?. Kama watu hawapimwi hiyo haina maana kwamba watu hawaumwi wala hawafi, kama watu wanaumwa na kufa kwa wingi unadhani bado wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wangekubali kuendelea na masomo?Unatumia kigezo gani kujua corona imepungua ilhali mlijichokea kwenye kupima, usipopima hauna namna ya kusema imepungua au la, unakua umewaacha watu wajihangaikie mitaani, wa kufa ajifie na wa kupona apone, na kwa nchi kubwa kama Tanzania ambayo media yake huwa imeminywa kuna mengi ambayo yatabaki kuishia huko kwa mtongole bila kusikika Dar.
Familia nyingi zinazoathirika inabidi wahangaike wenyewe ndani kwa ndani inabaki siri ya ndani maana ile wakijitangaza tu wanatengwa hata na jamii na kuepukwa.