The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Leo wizara ya Afya imetangaza kuwa hadi jana, tarehe 14, jumla ya watu 207,391 wamechanjwa kati ya chanjo 1,008,400 tulizoletewa na watu wa Marekani.
Chanjo zilizinduliwa rasmi tarehe 28 July, 2021, karibu wiki 3 zilizopita.
Tathmini yangu inajikita kwenye muitikio wa watu kuchanjwa. Leo hij karibu wiki 3 ama siku 20 watu 207,391 ndio waliochanjwa.
Hii ni wastani wa watu 10,369 kwa siku. Hii pia ni sawa na wastani wa watu 398 kwa mkoa kwa mikoa 26 Tanganyika.
Mpango wa Covax ni kusaidia kila nchi angalau chanjo ya 20% ya watu wake. Kwa Tanganyika tutahitaji chanjo ama tutapata chanjo milioni 12 kwani kwa takwimu za sasa zisizo rasmi tunakadiriwa kufikia milioni 62.
Sawa kwa huo muitikio ambao umeonekana kwa hizi siku 20 ina maana kumaliza hizi chanjo za mwanzo 1,08,400 itahitajika siku 96 ama miezi 3 kuzimaliza.
Kwa hesabu ya haraka haraka kama chanjo milioni 1 itahitajika miezi 3 kuzimaliza, chanjo milioni 12 itahitajika siku 1,142 ama miaka 3 kumaliza kuchanja watu 12m. Tukienda mbele zaidi inatakiwa nchi ichanje angalau 60 ya watu wake, yaani kwa Tanganyika watu 36m, hii itahitaji miaka 10 kumaliza kuchanja.
Kwa mtazamo wangu, chanjo ni muhimu inaokoa ama inasaidia baadhi ya watu lakini kwa Afrika chanjo ni usanii mtupu.
Ukweli ni kwamba kwa miaka 3 ijayo hakuna nchi Afrika itakayokua imechanja hata 30%. South Afrika wamechanja watu 5% kwa miezi 8 na ni nchi ambayo iko vizuri kiuchumi, miundombinu sembuse Tanganyika.
Hapa tunajidanganya tu.