data
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 26,858
- 23,768
Nimeshangaa..Saida kalori na maua.......wtf!!!!!!??????........
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeshangaa..Saida kalori na maua.......wtf!!!!!!??????........
Anaweza kuchukua nafasi ya kiba maana kiba teyali kashapotea ila sio mond, mondi ni habari nyingine.
.
Miezi michache kadhaa niliandika Makala maalum kuhusu Konde Boy Juu ya uamuzi wake kujiondoa WCB na vitu atakavyotakiwa kuvifanya ili kuweza kuwin soko nje ya WCB, Makala niliichapisha kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii nikiipa jina la (VITU VINNE VYA SANGUJ VITAKAVYOMPA TABU HARMONIZE NJE YA WCB.)
.
Kwanza lazima tukubali @Harmonize anaenda kumaliza vizuri mwaka, Kwa sababu ya Mambo ambayo nilidhani angeweza kuyafanyia kazi, na ameyafanyia kazi kweli sijui kama alisoma au nadhani Menejmemt yake mpya asilimia 90 ilikiwaza ambacho Mimi nilikifikiria.
.
Kwanza @Harmonize amejitahidi Kwa asilimia karibia 80 mpaka 90 kurejesha mahusiano yake na baadhi ya media ambazo, zilikuwa hazina maelewano mazuri na yeye, tumeona ameshiriki kwenye interview mbalimbali Kwa kituo kama @CloudsTV na wamempa sapoti ya Hali ya Juu Sana, tumeona ameshiriki Tamasha kubwa kama Fiesta na amekutana na Crowd mpya ambayo zamani hakuwahi kuwa nayo, pia amefanya promotions ya kutosha Sana ya kutengeneza Ufalme wake Kwa kufanya matamasha yake.
.
Japo nikiri kuna kitu kimepungua Kidogo ambacho nimekiona, moja ya vitu ambavyo Harmonize alikuwa anavikosa ni kufanya show chache sana ndani ya nchi, na kufanya show nyingi nje ya nchi lakini tangu atoke WCB nadhani zimepungua Sana za nje ya nchi sijui nini tatizo labda uongozi wake haujapokea maombi ngoja tuendelee kusubiri labda 2020 utakua Moto zaidi kwake.
.
Mimi Kwa maoni yangu Konde Boy amejitahidi Kwa muda huu mfupi ambapo ameishi nje ya WCB kwanza baada ya kutoka hakuruhusu mijadala mirefu sana Juu ya yeye kutoka WCB aliwataka watu waanze kuconcetrate na yeye Tu kama Msanii na si migogoro hii Hongera Sana.
.
Pili amekuwa Karibu zaidi na Serikali (Safi Sana) na imemjengea uaminifu Sana Serikalini na unajua ni rahisi kwake pia kupata sapoti kubwa pindi anapokuwa na Jambo lake kisanaa na hasa ukifikia msimu wa kampeni 2020, ukianza atakavyozunguka na Mgombea Urais wetu wa CCM Nchi nzima na hapo ndipo base yake itakapoongezeka zaidi simaanishi kwamba wasiokuwa Karibu wanapata ugumu hapana Serikali ya JPM ni sikivu Kwa wasanii wote bila kuwabagua chini ya Baba Mwakyembe.
.
Ninachojiuliza Kwa asili ya muziki wetu Tanzania, siku zote lazima kuwe na Mafahari wawili ambao hawakai zizi moja, ndiyo maana tuliona East Coast Team na Wanaume Family, Mr Nice na Dudubaya tuliona Saida Kalori na Maua, tuliona Lady Jaydee na Ray C na sasa Alikiba na Diamond Platnumz nawaza Harmonize ataweza kupenya kwenye Mafahari hawa wawili.
.
Naiwaza nguvu ya Alikiba na naiwaza nguvu ya Chibu najiuliza nani atashuka ili Fahari mpya Harmonize aingie kati, sijui ndiyo itakua kama Modric alivyoingia katikati ya Ronaldo na Messi halafu akapotea, nadhani Ngoja tuone 2020 itakuaje nadhani Tutaona Historia ikiandikwa tukaanza kuwa na Mafahari watatu.
.
Mwisho niliyoandika ni maoni yangu yasihusishwe na kampuni yeyote au mtu yeyote, na furaha yangu ni kuona muziki wetu unapiga hatua.
.
#KijanaMzalendo
#IloveTz
Instagram ; Facebook @ SanguJoseph
Sent using Jamii Forums mobile app
una point lakin watakubezaTuache Unafiki bwana, Dogo anapotea. Kusema kamaliza mwaka vizuri unamaanisha nini? Kutoa UNO na Kushoto/Kulia?
Kuona mafanikio yake nje ya WCB tufananishe na alivokua ndani. Sema ndio hivo baadhi ya data hatuwezi pata mfano kipato kwa mwezi, idadi ya shows kwa mwezi, mikataba nje ya music, etc.
Kupatana na Clouds na kushiriki Fiesta hakuna impacts kabisa katika mafanikio. Kwasababu mashabiki ndio wanaompa mafanikio msanii na sio Radio. Mtu kama Harmonize hakuna Mtanzania anaependa Music wa Bongo Fleva hafu asimjue, kwahiyo wimbo wake kupigwa au kutopigwa Clouds hakuna impacts kabisa. Labda uniambie Clouds inasikilizwa sana nje huko ambako radio nyingine hazifiki.
Tutaishia kumpima kwa likes za Insta na views za Youtube ambazo hazina faida kwenye mafanikio.
HaterTuache Unafiki bwana, Dogo anapotea. Kusema kamaliza mwaka vizuri unamaanisha nini? Kutoa UNO na Kushoto/Kulia?
Kuona mafanikio yake nje ya WCB tufananishe na alivokua ndani. Sema ndio hivo baadhi ya data hatuwezi pata mfano kipato kwa mwezi, idadi ya shows kwa mwezi, mikataba nje ya music, etc.
Kupatana na Clouds na kushiriki Fiesta hakuna impacts kabisa katika mafanikio. Kwasababu mashabiki ndio wanaompa mafanikio msanii na sio Radio. Mtu kama Harmonize hakuna Mtanzania anaependa Music wa Bongo Fleva hafu asimjue, kwahiyo wimbo wake kupigwa au kutopigwa Clouds hakuna impacts kabisa. Labda uniambie Clouds inasikilizwa sana nje huko ambako radio nyingine hazifiki.
Tutaishia kumpima kwa likes za Insta na views za Youtube ambazo hazina faida kwenye mafanikio.
Tena hapo alipojiingiza kwenye siasa itamcost huko mbele