Tatizo baada ya kupangiwa placement

Hujasema ni mtumishi wa kada Gani?

Ulitoka wapi kwenda wapi?

hughuli yako mahsusi ni ipi mwanzo na baadae kuwa ipi?
 
Penda Utumishi ukawaeleze tatizo lako kijana ikishindikana kaongee na Katibu Mkuu utumishi
 
Komaa hapo ukizubaa imekula kwako,kua mbishi kiaina.
Ishatokea kwa jamaa yetu CRB akakita barua ishachukuliwa,akakiwasha mwisho wa siku wakampambania kuweka mambo sawa,kumbe Kuna mutu alichomekwa,ila ni enzi ya JPM
 
Pambana mkuu usikubali kupokonywa tonge mdomoni kizembe hiyo ni haki yako ipambanie
 
Kuwa makini utapoteza hio kazi. Taasisi zina mambo yake.

Swali: Mwajiri alikupokea kwamaana ya kusajiri ujio wako ili aendelee kukushughurikia ukiwa kama mtumishi wake?

Barua ya kazi ilikutaka ulipoti kwa mwajiri ndani ya siku 14. Mara baada ya kuripoti siku ya kuripoti huhesabika rasmi kama siku ya kuajiriwa kwako. Kama mwajiri alikataa kukupokea rasmi, hio case ilipoti ofisi za juu hapo kwenye Taasisi.
 
Nenda mahakamani.
 
Mwezi wa tisa na sasa ni mwezi wa 12, fanya hivi tafuta mawasiliano na HR wa iyo taasisi muulize kinachoendelea juu ya swala lako asipokupa majibu ya kueleweka nenda utumishi kawaelezee swala lako wao watakusaidia ila inahitaji ukomae usionyeshe unyonge.

Ninavyofahamu ajira mpya ukienda kuripoti unatakiwa u submit barua yako pamoja na vyeti vyako ili uingizwe kwenye mfumo na unaweza kuanza kazi hapo hapo au unaweza kungojea kidogo kisha uitwe kuanza kazi

Sasa swali langu la msingi kwanini wakatae kupokea barua yako kutoka utumishi?

Maana yake hawakuchukua taarifa zako zozote (hawakukuingiza kwenye mfumo wao) si ndio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…