Tatizo baada ya kupata placement

Tatizo baada ya kupata placement

Habari wakuu samahani na poleni na mihangaiko ya kila siku, naomba ushauri.

Nilipata placement utumishi Mwezi wa tisa baada ya kureport kwenye taasisi husika wakaniambia nitapigiwa simu ila mapokezi katika taasisi hiyo ayakuwa mazuri maana walikataa ata kuchukua barua kutoka utumishi nikaambiwa nitapigiwa simu.

Mpaka leo kimya lakini wenzangu walio enda taasisi zingine wameshaanza kazi.

Mimi nipo tu, sina cha kufanya maana kila kitu kwenye maisha yangu kimesimama naomba ushauri juu ya jambo hili

Nichukue hatua zipi.
Placement ni nini mkubwa?
 
Wapigie utumishi! Wala usiharibu nauli yako, alafu utumishi watafanya mawasiliano yao! Vinginevyo utakaa hata miezi mitano! Kuna jamaa mmoja alipata kazi akafanywa hivyo hivyo mwisho wa siku akaambiwa nafasi hazipo ilibidi arudi utumishi akaambiwa asubiri gap lingine na kweli alipangwa baadaye lakini sehemu ambayo mshahara wake ni mdogo tofauti na taasisi ya awali! Maana huko ulikopeleka barua yamkini walishasahau mkuu! Na vile yawezekana ulitoka database ndo kabisa utaendelea kusugua benchi! Kumbuka hii sio awamu ya anko magu!
 
Habari wakuu samahani na poleni na mihangaiko ya kila siku, naomba ushauri.

Nilipata placement utumishi Mwezi wa tisa baada ya kureport kwenye taasisi husika wakaniambia nitapigiwa simu ila mapokezi katika taasisi hiyo ayakuwa mazuri maana walikataa ata kuchukua barua kutoka utumishi nikaambiwa nitapigiwa simu.

Mpaka leo kimya lakini wenzangu walio enda taasisi zingine wameshaanza kazi.

Mimi nipo tu, sina cha kufanya maana kila kitu kwenye maisha yangu kimesimama naomba ushauri juu ya jambo hili

Nichukue hatua zipi.
Aliyekataa ni nani? Au watu wa masijala?
Itaje iyo taasisi au nitumie pm
 
Back
Top Bottom