Tatizo hawakutaka kumsikliza Ferguson, acha Mino na mwanae Pogba waendelee kuwatesa

Tatizo hawakutaka kumsikliza Ferguson, acha Mino na mwanae Pogba waendelee kuwatesa

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
imeandikwa na Nasri Van Man Utd

Akiwa na umri wa miaka 18 ,Paul kijana mwenye kipaji asili cha mpira alianza kuwa gumzo kwenye mitaa ya Carrington , kama alivyowahi kusema mwanafalsafa mmoja kuwa Gorden fish has no hiding place… Akiwa anamaanisha kuwa samaki mzuri au kitu kizuri huwa hajifichi ; kipaji huwa akijifichi ,hata wakala wake Mino Raiora alijua mapema kuwa kuna kitu kwenye miguu ya Paul na ndio maana alianza kumjenga mapema kama brand ili aje apige pesa baadae
.
Paul Pogba anakipaji hasa, uwezo na maamuzi vinamfanya awe miongoni mwa wachezaji waliokamilika kisoka .. Ukiachana na umahili alionao kwenye kucheza mpira ,Paul anafeli sehemu kubwa ya maisha nje ya uwanja .

Achilia mbali kibuli anachopewa na wakala wake Mino. Paul amekua kama mtumwa wa akili yake … maaamuzi na fikra pevu vitamfanya akose thamani; wala kipaji akita msaidia chochote.

Kipindi Manchester United ipo chini ya Sir Alex Fergurson kilikua kuna matatizo kama haya, ni kipindi ambacho Paul ndio ameitwa kwenye timu ya wakubwa ,alikua hana uzoefu wa kutosha na alikua ajekomaa kisoka ; ninaposema kukomaa kisoka ninamaanisha uwezo,maamuzi pamoja na kipaji ..

Paul alikua na kipaji sawa … tunakubaliana kwa hilo , uwezo alikua amefeli kwenye kasi ,nguvu pamoja na ukakamavu … na mwisho alikua hana Maamuzi sahihi akiwa na mpira ..; alikua na kipaji lakini alitakiwa kujifunza zaidi …

Kipindi ambacho Paul anaibukisa kwenye uchezaji hasa eneo la kiungo kwenye klabu ya Manchester united ; alikuta inawachezaji eneo hilo wakali kama Paul SCHOLES ,Michael Carrick , sawa Paul scholes alikua anaelekea mwisho kutokana na umri wake .. lakini ilikua sio rahisi kwa kijana mdogo kama Paul kuanza kukabidhiwa mapema majukumju bila kufuata utaratibu ,inamaana Kiutaratibu Pogba angeanza kupata namba taratibu huku baadhi ya michezo scholes akiwa nampisha au anaanza.

Tuanza kwa Paul Pogba mwenyewe ,alianza kutoa maneno ya kashfa kwa baadhi ya wakongwe kama wakina Carrick na Scholes , akitupa madongo ya kuwa hakuna mchezaji wa kumpiga benchi , kwanza ni wachezaji Wazee, hawaendani na soka la kasi .. akiamini kuwa kwa kiwango chake hana hadhi ya kuwekwa benchi kutokana na wachezaji waliokuepo kikosini.

Kumbuka maneno haya anayatamka kwanza alikua ajafanya kubwa lolote kwenye soka ,kisha ni chipukizi ;yaani kijana mdogo na aliweza kuwatusi wakongwe aliowakuta .

Baada ya maneno kuanza kuwa makubwa ndipo watu na washabiki wa soka tukaanza kufuatilia kuwa ninani ambaye anaweza kuwa na jeuri ya kuongea utumbo chini ya kocha ferg . Kwa mara ya kwanza jina la Paul Pogba tukaanza kulifahamu .. kabla hata hatujaanza kumfaidi katika kile ambacho kilichokuwa kinazungumzwa kuhusu yeye; mara tukasikia Ferguson kamuuza bure kwenda Juventus .

Lakini kocha Ferg alikuja kufichua kwenye kitabu chake ni kwanini alimuuza Pogba .. Ferguson anasimulia kuwa ; kwa mara ya kwanza anakutana na wakala Mino Raiola aligundua hawezi kufanya kazi na mtu wa namna hiyo,tena anadai macho ya Mino yalijionesha mapema; na yakamuakilisha tabia yake iliyo mbovu .

Ferg hakuishia hapo na akaongezea ya kuwa ; Pogba alikua na mkataba wa miaka mitatu na kulikua na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine … lakini kutokana na wakala wake kuwa na tabia ya kuhitaji pesa; alivuruga mambo kiasi bodi nzima ilisimama … kila mtu alitamani kumjua huyo kijana ni nani … Maana hakuna mtu aliyekuwa akimfahamu Paul .

Kisha alimaliza kwa kutoa ushauri juu ya Pogba , alisema kuwa Paul ni kijana mwenye kipaji … tunasikitlika kumuachia kijana huyo, lakini kama kweli anandoto za kufika mbal ninamshauri aachane na wakala Mino Riola kwani anaonekana hana malengo mazuri .
Ferg aliona mbali juu ya Pogba , kwanza aliamini kwenye kipaji,lakini aligundua kuna mtu anampa kiburi Paul, kiasi anakosa mpaka adabu … kumbuka Paul aliwahi kuwatusi maligendi kama wakina scholes; kuwa awastahili kumuweka benchi akiwa mdogo kabisa …

Yaani ukimsikiliza Ferg vizuri juu ya wakala MINO utagundua fika asingeweza kufanya nae kazi … hata kama angekua anamiliki mchezaji mkubwa kama PELE … na kwa hili Ferg akuwa mnafiki aliwahi kusema wazi kuwa anmchukia sana wakala MINO RAIOLA .

Miaka kadhaa imepita baada ya mzee Ferguson kuachana na klabu ya Manchester United , kocha Josse Mourinho akiwa kocha mkuu wa Utd, wanamrudhisha Paul Pogba … safari hii akiwa staa mkubwa .. aliondoka kinda aliyekua anakua kwa kasi na anarejea akiwa amekamilika kwenye soka .. Mbaya zaiadi akiwa na wakala wake Yule Yule mzee baba Mino Raiola .. mpenda pesa na kiburi … unategemea nini ..

Tatizo la Paul ni MINO …. Hatukutaka kumuelewa ferguson … na sasa kila mtu anannza kuamini kuwa Paul ni kijana mwenye kipaji ila nyuma yake kuna mtu mshenzi .. anayempa kiburi na kumkosesha adabu.

Kuna mambo yanayoendelea juu ya Pogba na wakala wake ; yanakela ,yanaudhi na kushangaza .. kabla ya mchezo wa Manchester City vs Man united uliopigwa etihad msimu uliopita ,kocha Pep Guardiola alifichua siri kuwa wakala Mino alimuomba Pep amsajili pogba … yaani Pogba akiwa na msimu mmoja tu na united lakini wakala wake ameshaanza kumtafutia timu nyingine .. huu ni ujinga ulioje ..

Unaanzaje kumtafutia mchezaji timu nyingine akiwa bado hajarudhisha thamani yeyote ndani na nje ya uwanja … alianza na msimu mbovu , hakurudhisha thamani ya pesa alizonunuliwa zakuvunja record ya uhamisho, lakini hauoni hilo linaumuhimu ;wewe unachojali ni maslahi yako .

Hakuishia hapo ndani ya dirisha hili la usajili liloisha Mino alisafiri mpaka katalunya kufanya mazungumzo na Barcelona juu ya uhamisho wa Paul …
Sema Brca hawakuwa tayari kwa muda huo … na sasa kuna habari za kuwa anataka amrudishe mteja wake kwenye klabu yake ya zamani yaani Juventus .. huyu ndio Mino … jeuri anayekela …
Kwasasa ni kama ferg anacheka kimoyomoyo … anacheka kwa dharau akiamaini hawakutaka kunisikiliza juu ya Pogba na walaka wake ..
Kila kukicha klabu ya MAN UNITED imekua kama bongo movie … skendo kupita kiasi;hakuna kinachofanyika ; kisa pogba na wakala wake .
Pogba amekua ni Yule Yule …. Amekosa adabu ; kila kukicha amekua mitandaoni kulalamikia hana furaha,anataka kuondoka … na kama kweli kunamatitizona anataka kuondoka; kwanini asiache wakala wake na uongozi wamalizane .. Kiukweli Pogba na wakala wake walipofikia wanauzi ;wanakela na hawafai kuvumilika.

Kuhusu kipaji tunaungana na Ferg , paul nakipaji hasa .. lakini havumiliki kwa tabia zake . Kama alionesha kiburi akiwa kijana mdogo ,vipi leo hii akiwa staa .. ?

Na kama kweli Paul anahitaji kuwa bora na kupendwa na kila mtu kama alivyosema mzee ferg ,anatakiwa aachane na wakala wake Mino Raiola .. kwasababu hakuna timu itakayovumiilia tabia zao .
utd_degea-20180914-0001-01.jpeg
 
Back
Top Bottom