Pole sana kaka kwa sababu ndo msalaba wa maisha. Pengine mngepata muda muafaka kwenye mazingira tofauti na mlipo say take a vacation ku renew your honeymoon and your vows. Hapo mjadiliane si kwa maana ya kusuluhisha ugomvi lakini kwa mantiki ya kuandika upya aganao la upendo wenu! Kila mtu amtahmini mwenzake na utashangaa pengine na wewe umejikwa na kumkwaza. Ndoa zote zina changamoto zake na wahusika wengine wanamezea tu!
Mara nyingine ni udhaifu binafsi wa tabia na si kwa makusudi. Ungeweka kumbukumbu je anarudia baada ya muda gani ..je amejitahidi kutunza ahadi/sheria/kanuni kwa muda gani.. Lakini katika maisha bila kujali elimu mliyo nayo upendo haupimwi kwa vitu vikubwa bali kwa matendo madogomadogo sana. Je na wewe humsababishi ajikwaze katika hilo? Muwashirikishe na wasimamizi wenu wa ndoa katika hali ya furaha tu na wao wamape somo na kujadili mambo yanayowatatiza katika hali ya kawaida.si ya kutatua ugomvi maana hapo kila mtu atakuwa hayuko katika hali a kupokea.
Kwa kumalizia.. gharama ya kutunza ndoa ni kubwa mno in terms of upendo na majukumu na kwamba kama uleavyo mtoto na kuganga njaa yako inapokuuma- endela kusemezana nae na sio kumsema kila siku za uhai wenu.
Kuna movie moja inaitwa "Fireproof" itafute muione wote inaweza kukupa silaha za mapambanio ya kuimarisha ndoa yenu.
http://www.heartstonepictures.com/shop/product_images/h/140/fireproof__74826_zoom.jpg
Nawatalkia kila laheri na naomba feedback juu ya kutumia ushauri huu